Peterking1
New Member
- Jul 27, 2022
- 3
- 1
Habari waungwana,
Leo kidogo tupate nafasi ya kusemea mambo ya michezo hasa huu mchezo pendwa, mchezo wa mpira wa miguu. Kifupi tuseme mchezo wa mpira wa miguu kwa ngazi ya ligi yetu inafanya vizuri kwa ukanda huu wa Africa Mashariki. Hilo ni jambo la kujivunia.
Lakini pamoja na hayo kumekuwa na mwenendo usiyofaa wa waamuzi (marefarii) wenye jukumu la kusimamia mpira unapokuwa ukichezwa uwanjani. Kwa misimu miwili ya hivi karibuni hili limejitokeza sana katika waamuzi kufanya maamuzi sahihi.
Tumeona waamuzi wakifungiwa na wengine kuondolewa kwenye ratiba ya kuchezesha mpira wa miguu. Hili la waamuzi sasa imekuwa kero, makosa yale yale yanajirudia rudia kila mara.
Uamuzi mbovu, usiozingatia weledi, uamuzi wa haraka haraka bila kutulia na kuhakiki kilichotokea, vinapelekea mchezo wa mpira kupoteza radha. Kwani maamuzi mabovu hunifaisha baadhi ya timu na kuumiza zingine. Ikumbukwe mpira wa Tanzania kwa sasa unafuatiliwa kwa karibu bara Afrika.
Ikumbukwe kwamba kila timu ina haki ya kupata ushindi inapocheza vizuri na sio kushinda kwa kupitia mgongo wa makosa ya waamuzi. Ni kweli mpira ni mchezo wa makosa lakini makosa hayo yawe ni yale yanayotokana na ufundi wa uwanjani na siyo upofu wa waamuzi.
Ni vyema sasa waandishi wa habari za michezo hasa huu mchezo mpendwa na wachambuzi kwa pamoja tuzidi kupaza sauti zetu kukemea moja kwa moja. Ifike mahali tuache kuweka maneno kama vile "Makosa ya kibadamu". Waamuzi wengi wanajificha katika kivuli cha maneno hayo "Makosa ya kibadamu". Ifike mahali sasa tuseme wazi wazi kuwa wanakosea.
Tusipofanya hivyo basi hali itakuwa mbaya kwa mpira wetu na hata kwa waamuzi wetu. Hili limejitokeza hivi karibu hakuna mwamuzi aliyeitwa kuchezesha michezo inayosimamiwa na CAF hata ile ya wanawake tu hakuna mwamuzi aliyepata nafasi. Na tuache kusema "Mpira wetu kivyetu vyetu" hili nalo linaleta ukakasi katika utendaji.
Mwisho niseme marefa mnaharibu radha ya mpira kwa kigezo cha kusema ni makosa ya kibidamu. Chezesheni kwa haki mshindi apatikane kwa makosa ya kiufundi ya uwanjani na mshindwa ajue kuwa ni kweli amekosea kiufundi.
Ni mimi,
Mtoto wa Moro.
0682 527 228