Mpira sio mchezo wa kiungwana. Nimeacha rasmi kushabikia timu yoyote kutoka Ulaya!

Mkuu hiyo ni pointless kabisa mchezo wa mpira sio mieleka hakuna anaemvunja au kumuumiza kwa makusudi perhaps wawe na beef au chuki binafsi salah kaumia kwa sababu kakutana na more powerful player zaidi yake cheki profile ya Ramos

Kuhusu kutoshabikia timu za ulaya huo ni uzuzu wewe huna timu yeyote wewe ni mpenzi mtazamaji timu yako ipo kwa ndugu wales karia. Hata usiposhabikia huna impact you better shabikia mbao fc
 
Ndio matatizo ya kuanza kushabikia mpira ukubwani.
 
Walioharibu Mpira

1. Ramos, hovyo sana huyu jamaa

2. Refa kufumbia macho uuwaji wa Ramos, kamuumiza Sala makusudi

3. Golikipa wa Liverpool, magoli mawili kawazawadia Real Madrid
Kipa kazingua goli 1 tu....lile la kwanza ila mengine yote usimlaumu unamuonea
 
Wewe sio shabiki wa mpira, wewe ni mshangiliaji tu. Huna sifa ya kuwa shabiki hata kidogo. Hivyo achana na mpira kabisa fanya ishu zingine.
 
Umeona leo tu?? Mbona derby ya kariakoo yule beki alimtemea mate mwenzie, na refa alikuwepo anakodoa macho tu?
 
Ronaldo aliumizwa na Payet akatoka analia Ureno akabeba ndoo leo kaumizwa salah eti football sio mchezo wa kiungwana hili ni tukio la kwanza kwenye soka mkuu acha tu kushabikia huku hupawezi mlijua mnaishangaza dunia mkaja na matokeo mfukoni
 
nadhani mtoa Mada sio mtu wa mpira na huenda pia hufatilii ligi ya spain..

Ramos kucheza ile michezo ni kawaida yake so sioni cha ajabu pale... tena hapo kichaa mwenzie Pepe ameondoka
 
Walioharibu Mpira

1. Ramos, hovyo sana huyu jamaa

2. Refa kufumbia macho uuwaji wa Ramos, kamuumiza Sala makusudi

3. Golikipa wa Liverpool, magoli mawili kawazawadia Real Madrid

Hiyo namba 3:-
Huyo golikipa unaweza hisi alikuwa na Mkataba na Maaramia kama wale wa kwenye mchezo wa Cricket (MATCH FIXING)
 
Nilisema, watu kuwa na matokeo yao mfukoni wakati mpira hawaujui, baada ya mechi lazima wapoteane.
Uzi huu ni mfano hai.
 
Lile tukio hakuna refa ambaye angeweka mpira wa adhabu na kutoa kadi, kama unaujua mpira utaelewa namaanisha nini
 
sioni kosa la Ramos, nimeangalia hiyo incident zaidi ya mara tano, sijaona kosa la Ramos, sidhani kama he brought him down intentionally.
Sure upo sawa. Kosa kubwa limesababishwa na muangukaji mwenyewe, huwezi kuvutwa vile ukaanguka kama ndezi tena kwa kutanguliza mikono, wakati unajua kabisa ule ni mpira wa miguu....!
Povu ruska lakini kwa aliyekula gunia la omo tu.
 
Hapo sawa, mbinu zipo sanaaaa. Sema Mo ni mpole sana km mess, ila hii ya kumiss wc hata mimi imeniumiza mno daah.
Mbona mwenzake Messi anakutana na Sergio Ramos na Pepe karibu kila msimu na halalamiki??
Kheeee kheeeeee kheeeeeeeeee!!
 
Acha kabisa kushabikia soka, maana una moyo wa plastiki, hata huko utaumizwa mbaya
 
Kila kitu duniani hapa tunapaswa kuelewa kwamba kinatokea kwa mipango na sio bahati mbaya. Hata bingwa wa kombe la dunia anajulikana isipokuwa lazima tuhadaiwe na kucheza mechi zote ili ionekane bingwa kapatikana kihalali.

Katika dunia hii kuna secret service nyingi ambazo hufanya kazi kwa matakwa flani ili yatimie.Mnikumbushe kuanzia Jumatano nije na uzi wa kuzichambua sercet service hizo na ushahidi nitauweka hapa muone.
NOTE.Mshindi wa KOMBE LA DUNIA anajulikana tayari sis tuendelee tu kushabikia timu tuzipendazo ila BINGWA kashafanyiwa mchakato kitambo.Unahitaji uwe na akili nyingi mno kunielewa nachokimaanisha
 
Acha kushabikia timu za uingereza kwenye uefa zitakutoa roho, timu za uingereza ni malofa sana quality player wanawauza laliga wanabaki na temporary player halafu wanategemea kushindana nazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…