"Mpira umeisha", je ni sahihi?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Hakuna kitu ninachokichukia kama ukasuku. Tokea RTD kuanza kutangaza mechi za soka, nadhani mtangazaji hakuwa na maneno sahihi ya kuishia kutangaza hivo akatumia maneno haya ya "mpira umeisha". Kila mtangazaji wa soka mpaka leo, iwe wa radio ama tv, atayatumia pindi mechi ikiisha. Huwa najiuliza kwa nini hawabadiliki na kutumia maneno kama "mchezo umeisha au mechi imeisha"?
 
"Mpira umeisha", ni msemo unaomaanisha mechi imeisha. Tunaona nahau na methali zinaandikwa mtindo fulani, lakini maana ya maneno hubeba maana nyingine. Usifanye tafsiri ya moja kwa moja kama yalivyo maneno.
 
Nenda kule kwenye jukwaa la lugha, kuna wataalam wa kiswahili watakuweka sawa, hapa watakuzingua tu.
 
kabumbu /kipute finito. hili ndo la kiswahili fasaha kabisa. mimi ndo zee la lugha aka zee la nyeti
 
Unanikumbusha jamaa mmoja alikua anasema "kwanini kila kitu tuige wazungu? Mimi sisemi half time mimi nasema nusu wakati"
Hahahah
 
Ni sahihi, kwa kuwa maneno huwa na maana nyumbuliko, hata kusema 'naenda kutazama mpira' haimaanishi kuenda kuukodolea macho mpira, bali kutazama mchezo wote!
 
Kweli mkuu, mie huwa napenda watu wanaotafakari mambo na kupata ufumbuzi sio 'copy n paste'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…