Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Hakuna kitu ninachokichukia kama ukasuku. Tokea RTD kuanza kutangaza mechi za soka, nadhani mtangazaji hakuwa na maneno sahihi ya kuishia kutangaza hivo akatumia maneno haya ya "mpira umeisha". Kila mtangazaji wa soka mpaka leo, iwe wa radio ama tv, atayatumia pindi mechi ikiisha. Huwa najiuliza kwa nini hawabadiliki na kutumia maneno kama "mchezo umeisha au mechi imeisha"?