Mpira umeisha kwa Amani wanaodai Haki haikutendeka wanataka kuvuruga michuano ya AFCON.

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Watanzania hatujui kipaumbele chetu ni nini, Amani kwanza au Haki kwanza.

Baada ya mechi kwisha na Tanzania kutolewa kwa (1 - 0) na Morocco, wachezaji na benchi lote la ufundi walisimama wakimlalamikia refa kuwa hakutenda Haki, vile vile kuna Watanzania wanasema refa hakutenda haki kawanyima Stars penalty ya wazi.

Mimi nasema tumshukuru Mungu mpira umeisha kwa Amani kabisa, turudi nyumbani tujipange upya, wanaodai Haki wanataka kuvuruga Amani ya mashindano ya AFCON.

Tumuombe kiongozi wa msafara Paul Makonda awafikishie viongozi wenzake jinsi inavyouma pindi unaponyimwa haki yako.
 
Upo sahihi kabisa. Hivyo ndivyo CCM huwa wanashinda
 
Refa alikuwa huru na ameamua kwa haki kabisa, wanalalamika kwa sababu wamefeli
 
Amani kwanza, Refa hajashambuliwa. Kwanini Tuvunje Amani ya AFCON? Tujipange miaka minne ijayo. AMANI KWANZA HAKI NDO INAFATA.
 
Taifa ambalo halitendi haki kwa raia wake huku viongozi waliojipachika madaraka wakiwazodoa na kuwabagaza, halafu linaenda nje linadai litendewe haki.

Wananchi wakifanya maandamano wanauawa kama kuku, halafu wachezaji wa timu ya taifa wanataka kuleta taharuki na kufanya maandamano kisa hawajatendewa haki.
 
Nimefurahi sana Taifa star kufungwa. safi sana
 
Mungu akitaka kukufundisha kitu anatumia njia yoyote ili itakapofika wakati wa maamuzi magumu kama ya Venezuela husilalamike
Tumekuwa na mjadala mrefu wa kipi kianze kati ya haki au aman
Kwakuwa Mungu ni mwingi wa huruma bado ametumia timu yetu ya taifa kutufundisha kile kile tulicho kuwa tunabishania
Sasa ikifika wakati Mungu akanyamaza tusimtafute mchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…