Mpira unaweza kufanyika nje ya TFF?

Mpira unaweza kufanyika nje ya TFF?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kuna hayamambo TFF inafungiamtu kujihusisha na mpira. Nauliza kama mpira hauwezi kufanyika nje ya TFF. Mtu anaweza kuanzisha ligi ambayo TFF hawahusiki kwa lolote?
 
TFF kutoa adhabu ya kifungo cha nje watu wengi wanashindwa kuelewa mchanganuo wa hiyo kauli

Ishu ni kwamba TFF ni taasisi mama inayoshughulikia maswala yote ya mpira hapa Tanzania.

Mtu yeyote anayetoka hapa kwenda nje katika maswala ya kimpiea lazima apewe baraka na TFF kwasababu huko atakuwa anapresent maswala ya mpira kutoka Tz ambapo TFF ndio taasisi inayotambulika na FIFA

Ili manara aweze kufanya shughuli za michezo nje basi itamlazimu aombe uraia wa nchi nyingine ili awe muwakilishi wa taasisi ya kimichezo ya nchi hiyo aliyoomba uraia
 
Mpira wa miguu ni kitu kimoja cha ajabu duniani,ni kitu pekee ambacho dunia imekubali kuwa wamoja na kuongozwa na taasisi moja kubwa(FIFA)

Binadamu pamoja na ubishi wao ila kwenye huu mchezo waliufyata mkia na wote kuwa kitu kimoja.

Ona maandishi watu waligoma kuna maandishi ya kihindi,kichina,kiarabu na haya ninayotumia,lugha ndo usiseme zipo nyingi mno lakini kwenye football eti dunia nzima ikawa kitu kimoja
 
TFF inaiwakilisha Serikali ambayo ni nchi. Huwezi kufanya mpira bila registration ya TFF itakuwa kama kumsomesha mwanao apate elimu nyumbani bila kufuata utaratibu wa nchi ambapo matokeo yake utayaona mbeleni.

Jamaa na yeye kazidi mno kidomodomo as if mpira anaujua yeye tu wengine hapana wacha atulie kidogo kwanza - tena miaka 2 michache yule angepigwa 10 kabisaa.
 
.
1658405358094.jpg
 
Back
Top Bottom