Ifike mahali serikali iweke sheria ya kulinda taaluma ya utabibu
vinginevyo upotoshaji utakuwa mwingi.
kwa wenye taaluma walau ya huduma ya kwanza wataelewa
ninachokisema.Kule vijijini kuna mambo yanafanyika
kama huduma ya kwanza ambayo mwishowe humsababishia
mgonjwa madhara makubwa endapo hatawahishwa kuonana na daktari.
Naona hatari ya kumwachia kila mtu
kusema awazavyo akilini mwake juu ya mambo ya kidaktari
kwa kuwa amepewa jukwaa la kusemea
tukijakushtuka tutakuwa tumeumia.Ni vema mamlaka husika zikachukua hatua.