Mpoto: Mzee Ngosha wa Nembo ya Taifa alikuja kwangu kama 'chizi', tukafanya kazi, akatutoroka..

Mpoto: Mzee Ngosha wa Nembo ya Taifa alikuja kwangu kama 'chizi', tukafanya kazi, akatutoroka..

Aisee.

Kweli hakumuona kwenye TV alipoibuliwa na ITV?

Kilichomfanya leo ajue ni yeye ni nini?
 
Msanii Mrisho Mpoto ameshtushwa na msiba wa Mzee Ngosha kwa aina yake!

Kwanza hakujua kama ni mtu aliyewahi kufanya naye kazi. Pia hakujua kama alikuwa mzima kichwani au la! Amekuja kugundua baada ya taarifa za kifo chake..

Anakumbuka ushauri wake uliosindikizwa na ujumbe "Yachukulie maneno haya ni ya chizi kaongea''.

Kwa ufupi, kisa ni cha kusikitisha na kufunza.

Tazama dakika ya 2 sekunde ya 22 (huyo mzee mwenye kofia nyekundu).

View attachment 516653



Well, msomeni Mpoto;
------------
"Hii ni taarifa ya kunisikitisha sana kwenye maisha yangu ya Muziki naomba niwashirikishe ndugu zangu.

Nakumbuka kabla ya kutoa wimbo wa [HASHTAG]#SIZONJE[/HASHTAG] Nyuma yake nilitoa "NJOOUICHUKUE" huyu mzee alikuja ofisini kwangu kuniambia maneno mzito sana kwamba anapenda kazi yangu na alinitabiria mambo mengi mazuri kwenye safari yangu ya Maisha nanukuu "YACHUKULIE MANENO HAYA NI YA CHIZI KAONGEA".

Ombi lake lilikua moja tu alitamani kufanya kazi na Mimi, ofisi nzima ikamchukulia kama mzee aliyechanganyikiwa wakataka kumfukuza, mlinzi wetu Wa ofisi akasema msimpuuze mpeni nafasi.

Tulipompa nafasi ndiyo akatoa wazo la video ya wimbo Wa [HASHTAG]#njoouichukue[/HASHTAG] iweje, na akasema yule mzee Mshuba kikongwe Muuza Bangi ataigiza yeye mwenyewe. Tulicheka Sana maana wazo lake lilikua zuri na liliungwa mkono na Director Adamu Juma.

Sasa leo baada ya kuangalia kwa makini kumbe ndiyo Yule mzee aliyefariki leo Mchora Nembo ya Taifa. Natamani siku zirudi nyuma niongee nae Tena, roho imeniuma sana kwa kweli sijui hata nifanye nini.

Kibaya zaidi baada ya shooting alitutoroka hata hatukujua tutampataje!

Ndugu wa marehemu tafadhalini mtujulishe kuhusu mazishi yake! ".
-------------

Ni hayo tu!

Huu ndio unafiki wakutupwa ina maana siki zote hizi tarifa za mzee zinasambaa mitandaoni picha zake hakujua hilo leo kafa anajua hatutopata ukweli pengine alimdhurumu au vipi ndio anakuja na porojo zake
 
Et alitutoroka..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna mdau hapa amenichekesha anasema ameshindwa kutambua sura ya mtu hai ameweza kutambua sura ya mfu!
 
Back
Top Bottom