Mpox yafikia Kaunti 40, Watu 19 wafariki, huku Kenya ikijiandaa na tishio jingine la Ebola

Mpox yafikia Kaunti 40, Watu 19 wafariki, huku Kenya ikijiandaa na tishio jingine la Ebola

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Kenya sasa imerekodi visa 1,298 vya Mpox na vifo 19 katika counties 40, huku serikali ikiongeza maandalizi dhidi ya Ebola kutokana na kuendelea kwa mlipuko huo katika ukanda wa Afrika.

Takwimu za Ministry of Health zinaonyesha Mombasa ndiyo inaongoza kwa visa 452, ikifuatiwa na Nairobi yenye 320 na Busia yenye 115. Serikali imesema counties saba, hasa zilizo katika transport corridors, bado ziko katika hatari kubwa zaidi ya maambukizi.

Hii inaonyesha jinsi Mpox ilivyosambaa kwa kasi. Kufikia Mei 2026, Kenya ilikuwa imerekodi visa 1,119 katika counties 38. Sasa idadi ya counties zilizoathirika imefika 40.

Wakati huo huo, Kenya inalazimika kujiandaa na Ebola.

Ministry of Health imeongeza surveillance mipakani, uwezo wa laboratory testing, isolation facilities na Rapid Response Teams kutokana na mlipuko wa Ebola katika eneo hili. Serikali imesema Kenya bado haijathibitisha kisa cha Ebola.

Lakini maandalizi bado hayajakamilika. Tathmini ya serikali mwezi Julai iliweka kiwango cha preparedness ya Kenya kwa Ebola katika asilimia 66, huku mapungufu yakitajwa katika case management, infection prevention, wafanyakazi wa dharura na vifaa. Counties 25 zilitambuliwa kuwa katika hatari kubwa na kupewa kipaumbele.

Hapo ndipo swali linakuwa kubwa kuliko Mpox pekee:

Ikiwa Mpox tayari imefika counties 40 kati ya 47 huku Ebola ikiwa tishio la kikanda, mfumo wetu wa afya una uwezo wa kushughulikia outbreaks mbili kubwa kwa wakati mmoja?
 

Attachments

  • Mary-Muthoni-.png
    Mary-Muthoni-.png
    595.4 KB · Views: 21
  • taking-sample-from-person-with-mpox.webp
    taking-sample-from-person-with-mpox.webp
    284.9 KB · Views: 22
Back
Top Bottom