MPs warned over documents

MPs warned over documents

Siri za serikali lazima zilindwe haswa kwa kipindi hichi ambacho kuna msukomsukowa afrika mashakiri ambapo kila nchi inataka kuwa mbabe na kuhakikisha maslahi yake sasa watu kama kina slaa ndiotuwe nao kwenye afrika yamashariki --- hakuna kabisa haiwezekani
 
Wewe kama mwananchi mzalendo na mpenda maendeleo lazima kuheshimu nchi yako pamoja na taratibu zake hiyo ni pamoja na kuficha siri za nchi yako na kutetea nchi yako pamoja na wananchi na interest zao popote walipo na wakati wowote utakapotakiwa kufanya hivyo au kulazimishwa kufanya hivyo
 
Siri za watawala na chama chao cha CCM na mafisadi wao akina Chenge, Lowasa, Mzindakaya, Mkapa, Anna Mkapa, Mramba, Marehemu Balali, Yona, Mgonja, Karamagi, Rostam, Hosea na wengine wengi. Wala si kwa faida ya wananchi wa Tanzania. Tusidanganyane hapa. Every thing they do its for their own sake and not the so called Wananchi. Full Stop.
 
Last edited:
Ila na wao ni wananchi wanastahili kutunziwa siri zao kama wewe unavyotunziwa hata hivyo hao wengine kesi zao zikomahakamani na mahakama ndio inahukumu wewe huna uwezo wa kuhukumu kama unafikiri waliiba au kufanya chochote cha kuvunja sheria na una ushahidi peleka suala lako katika vyombo vya sheria --- hapo tukokwa maslahi ya nchi sio mtu mmoja mmoja au makundi ya watu au vyama au dini au kabila
 
Jana Waziri wa Utumishi wa Umma, Hawa Gasia alichimba mkwara kuwa watumishi watakaobainika kuvijisha habari au taarifa za serikali watachukuliwa hatua za kisheria. Alitaja sheria zinatakotumika kuwabana kadhaa ikiwemo ya Kuhatarisha Usalama wa Taifa. Hivi wadau, chukulia mfano Raia aliyechomozesha habari za wizi wa fedha za EPA, je huyu anahatarishaji usalama wa Taifa!!!!!. Kwa nini mtu huyu asipongezwe na kutunukiwa tunu ya kulipenda Taifa hili na Raia wake wanaoporwa rasilimali zao? Ama kweli CCem wameamua kwa dhati kuhakikisha kuwa dhuluma kwa wananchi wa nchi hii inaendelezwa kwa nguvu zote. Lakini Ipo siku upepo utageuka tu
 
Mkuu,

Sisi tusisubiri upepo, upepo ni sisi wenyewe tutakapoamua kulivalia njuga suala la serikali kujidhania ipo juu ya wananchi.

Watu wa sheria inabidi mtusaidie ktk hili, katiba yetu inasemaje. Maana suala la whistle - blowing ni nyeti na tukiwaachia hawa mchwa hivihivi vizazi vijavyo vitachimbua makaburi yetu na kuchoma mifupa yetu kutulaani.
 
Shy
nakusoma mkuu.
mwaga hekima mzee usiogope
ila nikidadisi kwamba leo ulipata kifungua kinywa cha bia ukatafunia embe nitakuwa nimekosea?
 
Siri za serikali lazima zilindwe haswa kwa kipindi hichi ambacho kuna msukomsukowa afrika mashakiri ambapo kila nchi inataka kuwa mbabe na kuhakikisha maslahi yake sasa watu kama kina slaa ndiotuwe nao kwenye afrika yamashariki --- hakuna kabisa haiwezekani
Wakati mwingine huwa nabakia kucheka tu.Hivi ni nini hicho ulichokiandika hapo juu mkuu.Yani hawa waliopewa dhamana wafuje fedha/mali zetu kwa kisingizio cha 'siri' kisha tuwanyamazie.Shy u serious??
 
alichokua anasema Dr. slaa asubuhi kuhusu nyaraka, alisema haoni usiri wa nyaraka za wizi wa mali za umaa. Hana haja ya kuvujisha siri za watanzania kwani naye ni mtanzania.

Mimi kilichonishangaza na kuniuma ni kauliza Lazaro Nyalandu. Sikujua ana misimamo ya kijinga namna ile. amemfahamu kwa karibu kwa muda mrefu lakini sikujua anaweza kutetea uozo hadharani katika umri ule. Ameongea na Dr. Slaa kwa madharau sana na kwa lengo la kuwaridhisha watu fulani katika serikali. Ameongea kama mtetezi wa serikali na mtendaji pia. Amejaribu kumuonesha Dr. Slaa kuwa yeye siyo chcohote wala upinzani. Swali nililolipata ni kuwa yeye Lazaro tangu ameingia bungeni ameifanyia nini hii nchi? amewahi kusema nini cha msingi zaidi ya kuonesha ujivuni na kuwa amesoma?

Lazaro amechukizwa sana na Slaa kutamka mishahara yao. amejaribu kutoa hoja za kizembe lakini bado slaa alisimama kwenye hoja ya msingi. Amemwita Slaa ni mwizi kama mwizi mwingine na anastahili kuwa jela kwa kuiba documents. zaidi sana amemwita ni mwongo juu ya madai ya maslai wanayopewa.

Kwa upande mmoja nilimizwa sana na kauli za Nyalandu, lakini kwa upande wa pili nilielewa kwa nini Lazaro huwa jinsi alivyo. Unapokaa naye, hana cha maana anachosema juu ya nchi, wananchi na taifa. Kauli zake ni za kujisifu tu alivyo na pesa, alivyo karibu na wakuu, anasafiri kiasi gani, nk,nk. hana mawazo yoyote ya kimapinduzi kama kijana. ni mtu anayeonesha dharau ya hali ya juu kuhusu watu wengine ambao hawajapata mwanga aliopata yeye. ngoja nisiseme sana....ila ukweli ni kuwa yuko bungeni kwa maslahi yake na anaimba nyimbo za wazee wa ccm katika ujana yule. hana hoja.
 
Hivi huyu si yule alikuwa Rais wa Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) miaka ile ya 90s? Alikuwa analia na kushuhudia na kuibuka mapepo? Akajitahidi kunishawishi ili nilie nikashindwa! Azidi kushindwa!!!!!....kumbe alitumia mgongo wa dini? Hakika wapo wengi.

Dr. Slaa usife moyo, tupo pamoja.
 
Siri za serikali lazima zilindwe haswa kwa kipindi hichi ambacho kuna msukomsukowa afrika mashakiri ambapo kila nchi inataka kuwa mbabe na kuhakikisha maslahi yake sasa watu kama kina slaa ndiotuwe nao kwenye afrika yamashariki --- hakuna kabisa haiwezekani

MHHHHHH!!!!!!!?????!!!!!!???????!!!😱
 
Serikali yatoa onyo kwa wabunge wanaoiba nyaraka za siri

Na Kizitto Noya, Dodoma

MBUNGE ambaye atakayebainika anatumia nyaraka za serikali kwa sababu yoyote ile atakabiliwa na hatua za kisheria bila ya kujali nafasi yake, Bunge la Jamhuri ya Muungano lilielezwa jana.

Lakini serikali imesema haijawachukulia hatua wabunge ambao wana nyaraka hizo na ambao wamejionyesha hadharani kuwa wanazo kwa kuwa inaelewa kuwa wana madhumuni gani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Tabora Mjini, Siraj Kaboyonga aliyetaka kujua endapo Sheria ya Kinga na Haki za Bunge, inamruhusu mbunge kushika nyaraka za siri za serikali.

“Sheria hii haimkingi mbunge na wizi wa nyaraka za serikali hivyo kama ilivyo kwa watu wengine ni kosa la jinai mbunge kushika nyaraka hizo,” alisema Ghasia.

Alipotakiwa kueleza serikali imewachukulia hatua gani wabunge wanaokuwa na nyaraka hizo na ambao wamejionyesha hadharani, Ghasia alisema: “Tunawajua, lakini hatujawachukulii hatua za sheria kwa sababu tunaelewa wana madhumuni gani.”

Ghasia alisema kuwa wabunge hao wamekuwa wakiiba nyaraka hizo kwa lengo la kujijenga kisiasa na serikali inalishughulikia tatizo hilo kwa kuchunguza vyanzo vya upatikanaji wa nyaraka hizo.

“Sasa maadam wenyewe wapo leo na wanasikiliza mjadala huu, ninaomba wajirekebishe, kwani ukweli ni kwamba wanavunja sheria kama ilivyo kwa watu wengine,” alisema Ghasia.

Ghasia hakutaja majina ya wabunge ambao serikali inawajua kuwa wanamiliki au wanaiba nyaraka za siri za serikali, lakini kadri siku zinavyokwenda, vikao vya taasisi hiyo ya kutunga sheria vimekuwa moto kutokana na kashfa mbalimbali zinazoibuliwa dhidi ya viongozi wa serikali.

Wakati fulani, mbunge wa Karatu, Dk Willbrod Slaa alisimama bungeni na kuonyesha nyaraka alizonazo huku akisema kuwa sheria inayozuia kuwa na nyaraka hizo haihalalishi wizi, ubadhirifu wa mali za umma na mikataba mibovu na kudai kuwa yuko tayari kukamatwa.

Dk Slaa ambaye alikuwa akizungumza wakati Bunge lilipokaa kama kamati, alisema anaifahamu sheria hiyo lakini anazitafuta nyaraka za siri za serikali ili kutetea maslahi ya Watanzania.

Alisema kitendo cha kuwa na nyaraka hizo kinaonyesha ni kiasi gani mfumo wa serikali ulivyoanguka na akahoji ni nyaraka zipi anatakiwa azitumie bungeni na zipi asizitumie.

Miongoni mwa kashfa ambazo nyaraka zake nyingi zinaonekana kuvuja ni pamoja na wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ambayo taarifa za wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni zilivuja hata kabla ya serikali kuanza kuchunguza.

Pia kashfa ya kampuni ya Meremeta kuwa ililipwa mamilioni ya fedha na Benki Kuu, huku kukiwa na kashfa nyingine ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development (LLC) na mradi wa umeme wa Kiwira.

Taarifa za siri za kashfa hizo zote zilivuja mapema na kutolewa ama bungeni au kwenye mikutano ya hadhara.

Katika swali lake la nyongeza, mbunge wa viti maalum, Rosemary Kiligini alitaka kujua endapo serikali bado inahitaji kuwachunguza wabunge hao wakati wanajulikana na akajibiwa:

“Pamoja na hali hiyo, bado tunahitaji utafiti wa namna wanavyozipata nyaraka hizo, kuna madai kwamba wengine wanazinunua kwa maafisa wa serikali lakina tunachowaomba wasirudie."

Alisema mbali na uchunguzi huo, serikali imeanza kuwabadilisha vitengo vya kazi maofisa wake inaowashuku kushirikiana na wabunge kutoa nyaraka hizo kabla ya kuwachukulia hatua zaidi za kisheria.

Mjadala kuhusu nyaraka za serikali, ulianzishwa na mbunge wa Matemwe Kheri Ameir, aliyetaka kujua katika swali lake la msingi kwa Wizara ya Menejimenti ya Utumishi ya Umma, endapo kuna watu waliokamatwa kati ya mwezi Januari na Desemba mwaka jana kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za siri za serikali.

Akijibu swali hilo, Ghasia alikiri kukithiri kwa vitendo vya wizi wa nyaraka za siri za serikali na kutumika isivyostahili, tatizo ambalo alisema kuwa haliwezi kupuuzwa na ambalo linastahili kuwekewa mkakati madhabuti kulimaliza.

“Nyaraka za serikali ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria mbalimbali... Sheria hizo ni pamoja na sheria ya Usalama wa Taifa namba 3 ya mwaka 1970, Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa namba 3 ya mwaka 2002, Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002 na Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma,” alisema na kuongeza:

Sheria hizi zinaainisha mgawanyo wa majukumu baina ya vyombo mbalimbali vya dola na unatoa madaraka ya kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria, watuhumiwa wa wizi na nyaraka za serikali.”

Alitaja baadhi ya mambo ambayo tayari serikali imechukua kudhibiti tatizo hilo kuwa ni kuongeza kiwango cha elimu kwa kada ya watunza kumbukumbu, kutunga sheria mpya za utunzaji kumbukumbu na nyaraka za taifa na kuweka mfumo mpya wa utunzaji kumbukumbu unaodhibiti ufunguaji na utekeleaji wa majalada na nyaraka kiholela

Mjadala huo umetinga bungeni huku baadhi ya wabunge wakiwa tayari wamejitokeza bungeni kuhoji umuhimu wa nyaraka ya serikali kuwa za siri kama baadhi yake zinatumika kulihujumu taifa.

SOURCE: Mwananchi
 
unajua sheria au waraka kama hizi ndizo huwa zina wa-provoke donors na kuchukua hatua ambazo Mkullo hatozipenda, ni akina Slaa kuwa Taarifa EU etc utasikia habari yake kwenye kikao cha au incase mtu afungwe kwa sababu ya huo waraka, itakuwa kama Yule Mwandishi wa Habari wa Iran aliye fungwa kwa ajili ya espionage, na sisi nguvu kama za Iran hatuna
 
Hivi huyu si yule alikuwa Rais wa Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) miaka ile ya 90s? Alikuwa analia na kushuhudia na kuibuka mapepo? Akajitahidi kunishawishi ili nilie nikashindwa! Azidi kushindwa!!!!!....kumbe alitumia mgongo wa dini? Hakika wapo wengi.

Dr. Slaa usife moyo, tupo pamoja.

Ungelikuwa unaenda kanisani na kitunguu
 
Ila na wao ni wananchi wanastahili kutunziwa siri zao kama wewe unavyotunziwa hata hivyo hao wengine kesi zao zikomahakamani na mahakama ndio inahukumu wewe huna uwezo wa kuhukumu kama unafikiri waliiba au kufanya chochote cha kuvunja sheria na una ushahidi peleka suala lako katika vyombo vya sheria --- hapo tukokwa maslahi ya nchi sio mtu mmoja mmoja au makundi ya watu au vyama au dini au kabila

Shy,

Kutunziwa siri zao ni sawa, lakini siri za aina gani?

Siku zote huwa naheshimu mawazo yako, ila katika hili, natofautiana sana na wewe. Kama hauna hoja soma tu halafu uondoke, subiri utachangia katika sehemu nyingine.
 
Whaat?..

Jamani hivi hawa viongozi wetu wazima kweli?

Hivi hawa ni wasomi kweli au wanatumia Siasa pia kufikia maamuzi ya aina hii..
Hizi Documents haziwezi kuwa Government classified ikiwa zinahusiana na UFISADI..
Hivi hawafahamu yaliyomkuta Nixon na Watergate? hawakumbuki Yalimkuta Carter na Iran Contra..

Haiwezekani hata siku moja nyaraka zinazovunja sheria (someone's madudu) kuwa government classifed document...kisha mtu azipeleke Bungeni mahala ambapo sheria za ammendiments za sheria zetu hufanyika..

Kisha huwezi kusema zinatumika kwa Political motives ikiwa viongozi wanaopingana na matumizi mabaya ya wadhifa yanatoka vyama vyote vilivyopo Bungeni isipokuwa nyaraka hizi humlenga mtu mmoja au kundi la watu wahisika.. Itakuwaje swala la Richmond liwe Politcal motivated - EPA, Rada, Kagoda na kadhalika yawe Political wakati kuna wabunge wa CCM na baadhi Mawaziri wa serikali hawafahamu kilichotokea hata nyaraka hizo zikapita kufunga mikataba mibaya kwa taifa letu.

Hivi kweli mipango ya UFISADI baina na viongozi kwa usiri wao inaweza kuitwa Government Classified Documents?

Elimu si Kigezo cha kuwa na akili Tanzania hii. Bora wale wazee wa Pemba wasiosoma wana uwezo wa kutumia akili.
 
Je inamanisha Kikwete, Pinda na Serikali ya CCM wameunga Mkono waraka huu Au ni Maneno ya waziri husika Pekee yake, maana siamini kama CCM wote ni wajinga kama huyu waziri husika.

........na Wale waliokomalia suwala hilo Bungeni kutaka wajibiwe.
 
Hivi huyu si yule alikuwa Rais wa Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) miaka ile ya 90s? Alikuwa analia na kushuhudia na kuibuka mapepo? Akajitahidi kunishawishi ili nilie nikashindwa! Azidi kushindwa!!!!!....kumbe alitumia mgongo wa dini? Hakika wapo wengi.

Dr. Slaa usife moyo, tupo pamoja.

Ndio huyo huyo ... siku hizi kamuoa Faraja Kota yule mrembo aliekua Miss Tanzania...
 
Siri za serikali lazima zilindwe haswa kwa kipindi hichi ambacho kuna msukomsukowa afrika mashakiri ambapo kila nchi inataka kuwa mbabe na kuhakikisha maslahi yake sasa watu kama kina slaa ndiotuwe nao kwenye afrika yamashariki --- hakuna kabisa haiwezekani

Tuzifiche ili tukiingia kwenye hiyo jumuiya tuibe na kufisadi? Kwani hizo tunazoambiwa siri zilizofichuliwa ni siri za wizi na si siri za kuhatarisha usalama wa Taifa. Una maana twende tukafisadi huko?
 
Back
Top Bottom