"I have lived and worked in the US using a Green Card for over 20 years,"- Dr.Mrema
..kama mama alikuwa viwanja miaka 20 na ana Green Card kwanini anyimwe visa?
katika sakata hili ni vyema kusikiliza pande zote mbili kuna kitu kina-miss hapa.Dr Mrema ni lazima aelewe kwamba kuwahi kuwa na Green Card kwa miaka 20 sio guarantee ya kuingia US,ina maana hiyo Green Card yake ilikwisha expire kama ingekuwa valid asingekuwa na sababu ya kwenda kuomba visa.
Kinachonishangaza mimi ni kwamba ina maana huyu Mama haku-renew GC yake , ina maana hata uwe umekaa miaka 20 legally huko US lakini sasa hauna Status na inabidi urudi dirishani Embassy kuomba visa kama mtu mwingine.
Kwa utaratibu wa uhamiaji huko US kuna Green Cards za aina mbili 1).Temporary (2yrs). 2).Permanent (10yrs) na hakuna Green card ya Miaka 20,kwa maana hiyo Dr Mrema alikuwa ana-renew GC yake mara kwa mara(inategemea aina ya GC kama ya Kazi,kuoa,Lottery,Ukimbizi,Arts) na hiyo Permanent Resident Card (GC) ya miaka kumi una option ya kuomba Uraia ukifikisha miaka Mitano,na kama hutaki una-renew na wanakupa Card nyingine ya miaka mitano.
Hata hivyo Dr Mrema alipaswa pia kupata Invitation Letter kutoka kwenye hiyo Hospitali alolazwa mwanae,huo ndio utaratibu wa US,kwani hata wanaokwenda kuchukua Maiti Huko US inapaswa waletewe invitation Letter na Funeral Home iliyomtunza Marehemu,nafikiri katika misingi hiyo mtoa viza ndio akaona asimpe viza Mama kwa ushahidi wa maneno bila vidokezo.
Ni kweli inauma na ukizingatia kuwa Mwanao ni mahututi,lakini pia ni lazima tujali taratibu za kazi za wenzetu.Natanguliza Pole kwa ndugu na Jamaa wa Marehemu..Lakini pia Dr kama anaona hakutendewa haki anaweza kuwakilisha malalamiko yake kwa State Department na Jamaa huko hufanyia kazi/uchunguzi malalamiko hayo!