The Legacy
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 5,879
- 11,318
Salam JF,
Leo kwa mara ya kwanza naomba nimtetee Rais wangu baada ya Tafakari kubwa kiasi. Huyu Mama ana maono mazuri ila shida iko kwa wateuzi wake na Machawa.
Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Mh Rais Samia akifanya mapinduzi ya Baraza la mawaziri,wakuu wa mikoa na kada nyingine za uteuzi. Kama mtanzania anaefikiri kiasi nikawaza Rais wetu anatafuta nini kwa hii tengua na kuteua?Jibu nikapata Rais anatafuta tija na ufanisi kutoka kwa wateule wake lakini haipati.
Ni kweli Rais ana nia nzuri ya nchi yake kuendelea, na unaiona kabisa akiumia jambo flani lisipoenda.
Kama binadamu huwezikosa mapungufu sababu hayupo mkamilifu na anaepatia mara zote.Hata Rais mwenye nchi inayoongoza kwa uchumi duniani anakosea.
Unaona kabisa nia ya Rais kuiongoza nchi kupitia taasisi imara,cha ajabu anapo wateua wasaidizi wake hawamsaidii Rais na mwisho analaumiwa yeye na sio wasaidizi wake.
Msaidieni huyu Mama, Hata kama angekua nani hawezi kuwa na jicho kila sehemu. Mambo mengine rais anashtuka yameshaharibika na kuanza kuumiza kichwa namna ya kuyaweka sawa.
Rais akikuteua umsaidie sehem kuwa muwazi kama huwezi,kuliko kupokea nafasi kisha ukavurunda na kumuacha mama wa watu anahangaika kukutengua na kuficha aibu ya chama na serikali.
Samia pia achana na hawa wafia chama watoto wa wakubwa na makada ambao hawana uwezo bila shaka wanakuangusha,akishapata mtu nafasi moja akakosea mara tatu hebu muweke pembeni.
Wasaidizi wapo wengi wenye mawazo mazuri,muda mwingine wananchi wanaona ni bora wakushushie lawama sababu ya wewe kuteua sura zile zile as if kuna watu ni special kukusaidia hata kama wakikosea.Lazima mteule wako achukue nafasi yako kwa uzito na kukubali kutumika kwa nafasi adhimu.
Kwanini Lawama kwa Rais moja kwa moja?
Tangu Enzi za Rais Magufuli sifa nyingi na asizo stahili Rais huwa anapewa yeye, mfano zahatati imepata dawa basi atasifiwa mpaka kufuru,wakati ni jukumu la serikali kutoa huduma bora za afya, na yeye bila unafki na woga anazipokea na kuzifaa sifa asizostahili.
Machawa wanamponza sana Samia na kumfanya atumikie sifa zisizo mhusu.Ajabu mambo yanapoenda kombo kwenye maadhi ya maeneo ya mfano wanafunzi kukosa madawati lawama zote huenda kwa Samia na hao machawa hukaa kimya mama akipambana na fedheha kwa serikali yake.Machawa ni adui namba moja wa Rais wetu.
Wateule msaidie Rais ipasavyo, mpuNguzieni mzigo Mama.
Mama Kataa sifa usizostahili kutoka kwa machawa.
Asanteni.