Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mdau wa michezo Furaha Dominic amesema amezuiliwa kuwa Mgeni Rasmi katika fainali ya mchezo wa mpira wa miguu katika ligi ya Kunduchi super cup kutokana na sababu ambazo amesema ni za kisiasa kwani alipata mualiko wa kuwa mgeni rasmi katika fainali hizo wiki tatu kabla lakini leo imeenda tofauti.
Akizungumza katika viwanja vya Mtongani Furaha amesema kuzuiliwa kwake kuwa mgeni rasmi hakujamfanya asishiriki fainali hizo kwani yeye ni Mdau wa Michezo na ameahidi kuleta furaha cup mashindano yatakayoshirikisha timu zinazocheza michezo mbalimbali kutoka mkoa wa Dar es salaam na mshindi wa Kwanza kuibuka na shilingi milion 20, mshindi wa pili milioni 10 na mshindi wa tatu milioni 5.
Hata hivyo mratibu wa fainali za Kunduchi super cup Jamal Jabil amesema wao walimkaribisha Furaha Dominic kuwa Mgeni rasmi na sio Mbunge Josephat Gwajima hivyo fainali hizo zimemalizika kwa kuwa na Mgeni Rasmi Michael Urio ambae ni diwani wa kata ya kunduchi na naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni na mshindi wa kwanza ameipuka na kitita cha shilingi milion 2 na laki tano na mshindi wa pili amepata kitita cha shilini milioni moja na laki tano.