"Hali ya nchi Tanzania ni ngumu, tete na ina utata (alisema Mzee Kingunge) ukitazama katika televisheni unaona askari polisi wanajiandaa kwa kujitokeza hadharani .... waziri wa mambo ya ndani .... wakuu wa mikoa na maDC wanatoa matamshi ya ubabe na vitisho ... "- hiyo ilikuwa mwaka 2016 miaka 8 iliyopita anasema Kingunge.
View attachment 3084368
Picha: komredi Kingunge Ngombale-Mwiru
Maneno hayo ya miaka 8 iliyopita yanatokea kiaina 2024 ingawa kuna 4R na midahalo kukimbia, wanachama 500 wa CHADEMA kushikiliwa na polisi siku ya Vijana Duniani , watu kuteka, kutupwa msituni Katavi Mpanda...