Mpya kutoka kwa Elon Musk

Cesar Saint

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
423
Reaction score
726
Habari wanajamvi

2018 February 6 ni siku ya kipekee kwa wadadisi wote wa masuala ya anga na ugunduzi wa ulimwengu kwani ndio siku kampuni binafsi ya bwana ELON MUSK iitwayo SPACE X wamefanya jaribio lao la kwanza kurusha kombora(rocket) yenye teknolojia ya juu kuzidi ile ya Saturn V iliyorushwa na NASA .



Picha ya Falcon Heavy

Shughuli nzima imefanyika katika viwanja vya Kennedy Space Center (KSC) sehemu ile ile iliyotumiwa na NASA Apollo moon missions pia kwa kazi za space shuttles;Shughuli hii ilichelewa kidogo kutokana na ongezeko la kasi ya upepo kwenye matabaka ya dunia kwa takribani masaa mawili lakini hili halikuwarudisha nyuma timu nzima ya Space X na hatimaye wakarusha rocketi yao ya Falcon Heavy .



UPEKEE WA FALCON HEAVY
Ukiangalia na mshindani wake wa karibu Falcon Heavy rocketi nyingine iliyowahi kutengenezwa na Space X rocket ya DELTA IV HEAVY hii yenyewe ilijumuisha gari maalumu la the "midnight cherry red" convertible lililofungwa kamera tatu kwaajili ya kutoa mwonekano mzima wa safari ;Gari hili you ambalo linamilikiwa na Elon Musk kitu kikubwa kilichoshangaza wengi ni uwepo wa mwanasesere anayechukua nafasi ya dereva aliyevalishwa mavazi ya kinajimu aliyepewa jina la STARMAN kutokana na wimbo wa David Bowie “Starman” akiwa ameshika usikani kwa mkono wa kulia na mkono wa kushoto akiuweka kwenye mlango .









Ikiwa na urefu unaokadiriwa kuwa wa ghorofa 23 hii ndio rocketi kubwa mpaka sasa kutoka kampuni ya Space X . Kitako chake kimewekewa nguvu na Core Boosters tatu zilizotokana na muundo wa rocketi ya Falcon 9 ambayo ilikuwa na injini 27 (injini 9 kwa booster) ambazo huchochea kwa wakati mmoja na kutoa uwezo wa takribani paundi millioni 5 na moshi mzito wa 22,819 kilonewtons wakati wa kuruka.



Mpango mzima ulikwenda kama ilivyotarajiwa isipokuwa booster ya kati ambayo ilikosea kutua katika kituo pangwa baada ya kurudi duniani baada ya kufanya mandingo yake (cosmic dance) ambapo booster mbili zilitua katika kituo cha jeshi la marekati kilichopo rasi ya Canaveral Air Force Karibu na Kennedy Space Center .



Lakini booster ya tatu kutokana na kubadilika kwa kasi ya upepo ambao ulivuka makadirio na kufika 300mph kutokana na injini mbili katika tatu kushindwa kuwaka kwa wakati wakati wa kushuka na hivyo kuharibu sehemu ya kituo (drone-ship landing pad) kituo kilochokuwa katika bahari ya Atlantic kilichopewa jina la “Of course I still love you”



Safari ya Falcon Heavy ni kuelekea katika Sayari ya Mars takribani masaa sita na dakika 28 baada ya booster ya mwisho kujitenga na kurudi duniani manuva haya yataipeleka Roadster katika njia katika mzunguko wa sayari na hapo kuwapeleka Starman na Cherry takribani 248 millioni maili(400 millioni kilomita ) kutoka duniani na itakuwa Mars-Earth Cycler na hii inaamini itapeleka Roadster karibu na Sayari hii nyekundu ijapokuwa uwezekano ni mdogo sana.





“Hili ni jaribio na kama litafanikiwa nadhani tutakuwa tayari kurusha satellite kwa mission inayofuatia” Mission hii inaweza kuwa katika kipindi cha kuanzia miezi mitatu mpaka sita.
Alisema Elon Musk

Nawasilisha.
 
Nimeona video ya Starman youtube.. nikahisi labda ni video za kutengenezwa tu!!
 
nilikuwa nimezoea kuona hizo booster zikirudi kwa maparachuti lkn nilivyoicheki video yake lahaulah! mzungu si mwafrika!.
 
Musk ni shida ana plan zake tatu kuu
1)kupeleka extended falcon heavy mwezini
2)by 2022 apeleke spaceship mbili mars na kuanza kuweka stationa kwa ajili ya mining, power nd lighting na 2024 apeleke spaceship nne kupanua makaz ya mars na hatimae watu kuweza kuishi huko. As mpaka now ashatengeza mtungi wa tani 2400 uliojaa liquid oxygen kwa ajili ya mission hiyo.
3)kusafirisha watu kwa kutumia rocket kutoka sehem mbali mbali duniani within a minutes.
 
Nasikia mzeebaba mkulu naye anataka arushe satelite tatu angani..
Nasikia ana project kubwa ya vinu vya nyuklia ambavyo vikikamilika tutauza umeme east and central africa..
Pia vinu hivyo vitatengeneza na makombora ya nuclear na pia ataanza kutest 'ballistic missiles mwakaniii[emoji23] [emoji23] [emoji23] ..
CCM hoyeee
 
hahaaa manina kwa kichwa kipi chenye kuwaza mambo mazito kama hayo ..tuendelee kuwa mashabiki tu ..maaana hakuna tunachokiweza zaidi ykula pilau na wali kwenye kampeni zetu
 
Wacha tuendelee kuvunja tofari zinazo tengenezwa ndani ya nchi
 
Hayo ni mapinduzi makubwa kwenye mambo ya anga wenzetu wamewekeza huko ila sisi hapa kwetu haijulikani hata tulipowekeza
 
[emoji2] [emoji2] kwa bajeti gani tuliyonayo yani..? Usitake mbwana mkubwa aje kuchukua pesa adi za kwenye vibubu vyetu chini ya uvungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…