ENANTIOMER
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 1,419
- 804
hii itawahusu wale ambao walifanya transfer kupitia vyuo husika.
Itakula kwao.
Taarifa yenyewe ni hii hapa:
Tume ya vyuo vikuu tanzania (tcu) ina mamlaka kisheria kusimamia na
kuratibu udahili wa wanafunzi wote wanaojiunga na vyuo vikuu vyote
nchini tanzania.
Tume imebaini kuwa, hivi karibuni baadhi ya vyuo vikuu vimekuwa
vikitangaza kudahili wanafunzi moja kwa moja kupitia vyuo vyao kwa
mwaka wa masomo 2014/2015. Ifahamike kuwa, utaratibu unaotambulika
kisheria ni wa kudahili wanafunzi kupitia tume ya vyuo vikuu tanzania
na si vinginevyo. Hivyo mwanafunzi atakayeomba na kupatiwa udahili
kupitia chuoni moja kwa moja, udahili wake hautatambulika.
Tume inapenda kusisitiza kuwa waombaji wote wenye sifa za kujiunga na
vyuo vikuu wanapaswa kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa na
tume.