zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
MWK, Sheria ilibadilishwa na mafisadi waliopeana ruhusa ya kukupua mali za Watanzania kila kona ya Tanzania. Walikubaliana kwamba watakaposhtukiwa kama wanaiba na kusaini mikataba mibovu basi wakirudisha walichokipata karika ufisadi wao mambo yote yatakuwa shwari.
Huu ni usanii wa hali ya juu, wabunge wa CCM wangechachamaa wahusika wote wa kashfa ya EPA, Richmond n.k. waswekwe rumande wakati uchunguzi unaendelea basi nina hakika hilo lingetokea.
Wabunge wamebwabwaja hakuna chochote kilichofanyika watuhumiwa wote bado wako huru wakiendelea kufaidi mapesa yao ya ufisadi.
Nilishangaa kusikia bunge limeahirishwa hadi April. Mtaahirishaje bunge wakati nchi imegubikwa na kashfa nzito nzito chungu nzima, kwani wasingweza kuitisha kikao cha dharura cha bunge hata cha mwezi mmoja ili kuhakikisha watuhumiwa wote wanaswekwa ndani!? Usanii kila kona, halafu Chiligati atakwambia wao CCM ndio waliwawajibisha mafisadi! wakati bado wako uraiani wanapeta!
Tatizo kubwa ni watu hawaelewi maana ya kufata sheria na kuwa dikteta ndio maana unaona mambo mengi yanawashinda kuyatatua, JK anafata sheria na hawezi kuamka akajitolea maamuzi kichwani, kamata yule weka ndani, huyu kaiba sweka jela. Anafanya shughuli zake kiumakini na kwa utaratibu unaokubalika kimataifa, ndio maana leo hii unaona kina lowassa, ingawa wengi wanaelewa kuwa ni rafiki yake mkubwa, wanasota nje ya uongozi. Unataka kuniambia amkamate amsweke jela wakati tayari kuna tume ya Bunge inashughulikia maswala hayo? Apingane na Bunge? huo utakuwa ni udikteta.
Hali kadhalika kwa EPA, makampuni yanajulikana na humo inawezekana kabisa kuwa wamo waliokopa kwa nia safi na wamo waliokopa kwa nia ya kutorudisha, huwezi ukakurupuka na kuwakamata uwasweke ndani, utapata faida gani ukisha wasweka? Utakosa pesa na utaendelea kuwalisha bure jela. At the same time ukitumia busara kidogo utazipata pesa zitakazoweza kupatikana, utazipata mali utazoweza kuzishika na kuna uwezekano mkubwa wengi wakaanza kurudisha, na hili la kuzipata fedha na mali ndio kipaumble. Na yote hayo lazima ayashughulikie kisheria, akienda kimsobe-msobe kama unavyotarajia, atajikuta hana alichofanya ila ni hasara juu ya hasara.
Tumeona jinsi Mkapa alivyokuwa akikalia maamuzi ya kushughulika na ufisadi kwa makusudi kabisa. Na kwa muda mfupi tu wa awamu ya nne tunaona jinsi JK anavyo yashughulikia masuala ya ufisadi ulioanza mbali sana. Na nani asiyeyaona mafanikio ya uongozi wake?. Asiyeona nadhani ana matatizo, kama si ya nanihii basi ni ya nanihii.
Kama tunaongelea unazi tu, haya tuendelee. Waswahili wanasema nyota njema huonekana alfajiri.