Mr:Blue ATUPIWA VYOMBO NJE,ni ndani ya nyumba ya NHC

Mr:Blue ATUPIWA VYOMBO NJE,ni ndani ya nyumba ya NHC

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
35,771
Reaction score
4,065







Familia ya staa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr. Blue’, imeingia kwenye kashikashi baada ya kuvunjiwa nyumba na kutupiwa vitu nje, Risasi Jumamosi linashuka nayo.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘mwandishi’ wetu lilijiri Januari 30, mwaka huu, Posta, jijini Dar katika Ghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambayo Mr. Blue alikuwa amepanga na ndugu zake akiwemo mjomba wake (jina halikupatikana).

Kwa mujibu wa chanzo makini, Mr. Blue na mjomba wake walipangisha chumba kimoja kwenye ghorofa hiyo kwa miaka mingi iliyopita kisha wakaamua kuiba chumba kingine ambacho kilikuwa hakina mpangaji.

“Walitoboa mlango kwenye chumba ambacho kilikuwa hakitumiki, wakaanza kukitumia bila kukilipia hivyo jamaa wa NHC walipotimba wakatoa vyombo vyote nje,” kilisema chanzo.

Ilifahamika kuwa siku ya tukio wamiliki (NHC) walivamia na kuvunja mlango kwa kuwa Mr. Blue hakuwepo na aliporudi alikuta zoezi la kutoa vyombo likiendelea.

Alipoulizwa na Mwandishi wetu aliyefika eneo la tukio, kuhusiana na sakata hilo, Mr. Blue alikiri kutolewa vyombo nje na kudai hakuna tatizo kwani alivipelekwa kwa mjomba wake


 
Yani bado anaishi kwenye nyumba za kupanga tu?
 
Wasanii wetu bata kw sanaaa wanasahau mambo muhimu
 
Mmmh! C kuna nyumba alijenga kwa ajil ya marehem mama yake c akakae xaxa..ama zilikua sound tu!!!
 
Yani bado anaishi kwenye nyumba za kupanga tu?
We unashangaa nyumba ya kupanga, si asvali ya huyo, kuna king kong mmoja anaishi nyumba ya bibi halafu kuna watu humu wanaona sawa tu.... Ndo maceleb wetu hao. Wao ni mavazi na magari kwa kwenda mbele..
 
We unashangaa nyumba ya kupanga, si asvali ya huyo, kuna king kong mmoja anaishi nyumba ya bibi halafu kuna watu humu wanaona sawa tu.... Ndo maceleb wetu hao. Wao ni mavazi na magari kwa kwenda mbele..
Mbona matajili wengi wa kihindi wanakaa nyumba za kupanga?
 
Arudi kwa mama ake akalelewe upya
 
msanii=Bongo Fleva
gazeti=Risasi

hizi habari huwa nasoma nikigombana na my wife wangu kupunguza stress.
 
Back
Top Bottom