Mr Blue (baycer) the special thread

Mr Blue (baycer) the special thread

Huyo Mo rocka kuna siku nilikutana nae mitaa ya sinza,
Mimi nilikua na mishe mishe zangu natafuta bodaboda ili niwahi mara naona jamaa anapita na bodaboda yenye namba nyeupe huku amevaa vesti, mimi sikumjua nikamsimamisha kwa makelele kabisa, badabodaaa! Kajamaa kakageuka kakaniangalia kwa dharau kisha kakaondoka.
My take: mastaa jaribuni kujiweka katika muonekano walau wa tofauti kidogo.

Hahahaaaa inaonekana alikasirika balaa....
 
Hahaaaa uwe unatumention basi jamani hivihivi hatuoni hadi tupitepite...lol
Anyways,namkubali sana msela wa kino ana swaga flani hivi za kinyamwezi sitaki kukumbuka enzi za blue blue,mapozi....
Zaidi ni hii video yake ya pesa namuona Kiba pale...hatari sana
Coco beach naona pale

Hatuna haja ya kufanyia video south Africa tunafanyia hapa hapa bongo tu then inakuwa bonge la video
 
Hii ni kwa mashabiki wote wa huyu msanii wetu tuje tuungane kwa pamoja ww ni kama shabiki wa mr blue a.k.a baycer karibu kundini

Dogo anajua sana album yake kwanza uliwahi kuimiliki??
 
Hapana mkuu,unayo nn?

Nilikuwaga nayo enzi za cassete mwaka 2004 ni moja kati album nzuri kibongobongo nyimbo kama mapozi, kiss, Mr blu ,hiphop, na moja alifanya na Noorah ni za ukwli kinoma
 
Nilikuwaga nayo enzi za cassete mwaka 2004 ni moja kati album nzuri kibongobongo nyimbo kama mapozi, kiss, Mr blu ,hiphop, na moja alifanya na Noorah ni za ukwli kinoma

Blu alitoa album yake ya kwanza akiwa na miaka 16 tu ila midude iliyomo mule watasubiri sana yaani alikuwa kama drake anaimba na anachana sema chuki za wabongo kwa vile alikuwa anapendwa na mademu mkamuanzishia majungu mpaka kikosi cha mizinga kwenda kumtolea posa
 
Hahahaha mkuu hapo umeuwa
 
Yaaani mpaka sasa hivi sijajuwa kwa nn wasanii wengi wa bongo wanafanyia video zao nje kwa mfano ndomo location za South Afrika ina maana bongo location zimeisha ama?
 
Blu alitoa album yake ya kwanza akiwa na miaka 16 tu ila midude iliyomo mule watasubiri sana yaani alikuwa kama drake anaimba na anachana sema chuki za wabongo kwa vile alikuwa anapendwa na mademu mkamuanzishia majungu mpaka kikosi cha mizinga kwenda kumtolea posa

naikumbuka hii ya kutolewa mahari ila bluu yule wa mapozi,sema sijui starudi lini
 
Mr Blu kafanyiwa bureee video ya PESA

“Adam Juma from nowhere, ni mtu ambaye
sikuwahi kufikiria nitafanya naye video.
Nilishajaribu kutaka kufanya naye lakini
mipango ikawa haikamiliki. Alinipigia simu
mwenyewe namshukuru sana Adam Juma
na Mungu akusaidie kwa kunipa video bure
kabisa! Yaani video kila kitu bureee kabisa.
Mimi nasema kuishi na watu kwa upendo
ndo zimefanya hivyo ninaweza kusema ni
zawadi.”
 
Blue enzi hzo bana! Sasa anafunikwa mpaka ns maunderground!

Ulikuwepo FIESTA pale leaders? Mi nilikuwepo, nakupa ushuhuda kwamba japo Mr.Bluu hasikiki redioni kama zamani but still anapendwa sana, alipopanda stage aisee alipata shangwe za hatari sikuamini. Anyway maunderground gani wanaomfunika? Maana sikuile kulikuwa na mastaa wakubwa bongo walio hot kwa sasa but aliwapoteza alipopanda jukwaani
 
Back
Top Bottom