Mr. Blue: Wema Sepetu na Naj walinifilisi Sana

Mr. Blue: Wema Sepetu na Naj walinifilisi Sana

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.
“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.
“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.
Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.
Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.
 
ndiomaana kuna levels,hawakuwa level yako hao.ndio maana wakina clement wanaonga mpaka nyumba na hawalalamiki
 
ndiomaana kuna levels,hawakuwa level yako hao.ndio maana wakina clement wanaonga mpaka nyumba na hawalalamiki

Kuna wanawake wengine husipokuwa makini wanakufirisi mfano hao aliowataja blue ni watu wanaopenda sana matumizi na kujionyesha wanazo ata kama hawana kazi ya kueleweka,upenda kuiga hakina KIm
 
Mbona mr blue ni kama son kwa wema?
kweli sichagui sibagui atakaenizika simjui.....
 
pole sana dogo!ulikua mdogo sana kipindi kile ila yote maisha yamepita malizia kibanda chako upate usingizi wako.
 
Si ulikuwa unaona sifa kutoka nawema kisa katika kutwaa taji ili uandikwe sana nadhani hata wema hakukumbuki kwenye list yake maana ni ndefu
 
Mr.blue anakula NGADA,dogo hamidu anamwaribu huyu na alikua punda mr blue naona safari za nje zimekata
 
Ukiona umefanya matumizi alafu roho ikakuuma uje wewe bado unalazimisha tu......mbona ukinunua soda roho haikuumi......kila kitu kina stage zake....


Wallah...hili ni neno la siku...
 
Ukiona unatumia gharama kuuubwa ili tu upate coomer, basi ujue ni muhanga wa domo zege.....wajanja wanapiga hizo mambo kwa gharama za kawaida tu, alafu wanawaachia kina clemente na Diamond warekebishe......
 
Ila Blu simuelewielewi ukaribu wake na dogo Hamidu.

Kweli aise, huwa napata shida sana kumuona Blue anakuwa karibu na mtu aliyepinda kiasi kile...Dogo Hamidu ni jamii ya kina Dudu Baya, Kala Pina....Blue anatakiwa KUchill na kina Barnaba, Amini, Ommy........
 
Mbona mr blue ni kama son kwa wema?
kweli sichagui sibagui atakaenizika simjui.....

Sindano inashona koti, ila hata wema ni mwili tu nakumbuka enzi zile anasoma akiwa na bwana wake wa kama mwarabu fulani kila jioni lazina wapite naye kwa mguu maenei ya Meeda.
 
ndiomaana kuna levels,hawakuwa level yako hao.ndio maana wakina clement wanaonga mpaka nyumba na hawalalamiki

hao warembo atuachie sisi tunaohonga marange rover na ma bmw....!
 
Sasa Blue vihela vya club one night stand analalamika wenzake wamehonga gari wametulia tuu.
 
Back
Top Bottom