Mr. Nice apongeza kufungiwa nyimbo za wasanii zisizo na maadili

Mr. Nice apongeza kufungiwa nyimbo za wasanii zisizo na maadili

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Tuheshimiane’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa hatua hiyo ni sawa kwa sababu nyimbo hizo zitaharibu vijana na watoto ambao ndio wafutialiaji wakubwa wa muziki.

zzzzzzzz-1.jpg


“Unajua vijana, watoto wadogo ndio wanapenda zaidi muziki sasa hivi, mimi kama msanii nikiimba kitu ambacho hakina maana, mantiki, adabu ni vibaya,” amesema.

“Serikali inaona ni ajira yako lakini isifike maali ukachafua watu wengine, ni afadhali wewe samaki mmoja ukatupwa wengine waendelee kuchanua, sio wote waonekana wameoza,” amesisitiza.

Wiki iliyopita Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na nyimbo hizo kufungiwa. Miongoni mwa wasanii nyimbo zao zilizofungiwa ni Diamond, Nay wa Mitego, Snura na Roma.

Chanzo: Bongo 5
 
Fagilia bongo - mr nice

Bongo bahati mbaya - young dee

Naona dogo alikua anampinga ajuza mr nice...
 
Huyu nae roho mbaya inamsumbua tu,sasa Kuku kapanda baiskeli,fagilia na nyinginezo za enzi zake zilikuwa na maadili?
 
Mr. Nice kasahau hamornize kumuweka mjini... [emoji15] [emoji15] [emoji119]
 
Back
Top Bottom