Mr. Nice: Harmonize usirudie tena kuiba kazi yangu bila ridhaa yangu

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Msanii legend wa music wa bongofleva Mr Nice ameshangazwa na msanii Harmonize kuchukua vionjo wa wimbo wake kin'gasti Kwenye wimbo "Hainistui" bila kuniomba wala makubaliano.

Wakati Mr Nice akihojiwa amefunguka unajua kuchukua vionjo au beat au mistari ya msanii mwingine kwa kumuomba au kuingia makubaliano naye si jambo mbaya ni jambo zuri maana unakubali kazi ya mwenzako na hata wasanii wakubwa wa Marekani wanafanya hivyo kuliko hata sisi lakini wanafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za haki mimiliki ila huku bongo baadhi ya wasanii hawazingatii hili sasa ukitumia kazi ya mwenzako bila ridhaa yake huo ni wizi.

Ameongezea pia, namtaka Harmonize asirudie huo upuuzi tena nimemsamehe akirudia tena sitamuonea huruma nitamchukulia hatua za kisheria.

Hivi karibuni pia Harmonize alichukua beat na vionjo vya msanii Steve simple the boy bila ridhaa yake pamoja na msanii mwingine kutoka Kenya ikapelekea kutokea mzozo miongoni mwao.
 
Kurudia nyimbo ya mtu si kosa au sio kwamba umekosa ubunifu ila uwe umefuata sheria au umfuate muhusika,kama hujamfuata muhusika utakuwa hujafanya uungwana.

Mngt ya Harmo wawe makini hii ni mara ya pili,siku wanaweza kumpata mtu mtata ikala kwao.
 
@Basiliser,Si kweli. Sampling kwenye muziki ni kitu cha kawaida sana.

Hivi Jay- Z alikuwa amekata pumzi alivyofanya ile '03 Bonnie and Clyde yenye vionjo vya me and my girlfriend ya pac?
Ni vile tu msanii amevutiwa na kionjo cha kazi ya mwenzie. Suala ni kufuata utaratibu.

I moved your cheese!
 
Unafikiri anachukua kienyeji enyeji
Taratibu zinafatwa mzee

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona msanii anachukua vionjo vya wasanii wenzake..ujue pumzi imekata sema ni kufosi kingi ili aendelee kuwepo..tunaita kutembelea nyota.

#MaendeleoHayanaChama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe Diamond anavyogongea Kurudia Nyimbo za Wenzake Pumzi Imekata pia mkuu,.?

Huo ujinga Umenunua Duka Gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…