Mr Nice kawa dereva wa bodaboda?

Mr Nice kawa dereva wa bodaboda?

Mbona ze komedy walisha tangaza kufilisika kwake

Toka enz hiyo
 
Kwa hiyo ndo unataka kusema jose chameleone nae atakuja kuendesha boda acha hizo bosi!Hata huyu mshikaji anaweza kurudi na kuwa kifaru mkubwa tu!Mapambano ya maisha si yanaendelea!Hakuna mbaya yeye alisongeshe hivo hivo atatoboa tu!
Tumuombee Mungu arudi kwenye charti aisee.....
 
Sio hatari ni kazi km kazi zingine.
Ila jamaa si alikuwa celebrity ana mpunga mrefu.
tujifunze tu kupitia kwake kwa mabaya na mazuri yaliyomtokea

Mambo ya kawaida hayo cha ajabu nini ?? Si bora ajitafutie ridhiki yake kihalali kuliko kuiba?? Paul Gascogoine sasa anaishi kwa best yake na alikua millionaire, hamna cha ajabu hapo ndio maisha hayo kuna kupanda na kushuka!
 
Nitafanya hivyo mkuu ila na mimi niombee nifikie utajiri alokuwa nao hata kama nitakuja kuendesha boda poa tu!
Utajiri mkubwa una siri nyingi sana.

Ila ukitaka kufanikiwa mafanikio mazito kwa haki huku Afrika inabidi umtegemee Mungu sana aiseee.

Sarakasi ni nyingi mno.
 
Msilaumu maisha kama amefilisika "kweli" basi lawama apewe yeye mwenyewe Mr. Nice. Watu tunakuwa wa ajabu sana kila kitu lazima tutafute pa kuangushia lawama. Mara "Maisha" mara "shetani" mara "wachawi" kila mtu ana anatafuta pa kuangushia lawama.

Maisha yako ni matokeo ya matendo yako, hakuna wa kulaumiwa zaidi yako mwenyewe. Na wale wanafiki wanaojifanya wanaouliza "cha ajabu kipi" kwa Mr. Nice kufilisika mpaka kufikia kuendesha "boda boda" lazima watakuwa na wanamatatizo kichwani au zaidi ya hapo.

Ni pa kujifunza ukipata pesa usiwekeze kwenye dhima "liabilities" wekeza kwenye mali "asset" zitakazokuletea pesa kukidhi mahitaji ya kila siku. Mkipata pesa ni baloon, mark x, gambe, pamba, wakina Lulu kwanini usije kuendesha boda boda baadae.
 
ndo tunapoona umuhimu wa kuwa na nidhamu na kazi, naskia jamaa alikua anatupatupa ana pesa na ulevi wa kupindukia wacha avune alichopanda pia iwe fundisho kwa wengine.
 
Ni muda wetu sasa, kila mtu na muda wake usistuke na wwe kuja kua bodaboda siku zingine.
 
bei ya bodabda nadhani ni kama nilioni 2 so kuliko azitumbue amefanya la maana hapo japo picha ingeleta utamu wa uzi pia
 
Subaiiii

Eti naskia jamaa anaendesha bodaboda kweli maisha yanashuka na kupanda.
dah! Bora aendeshe hyo bodaboda kuliko kukaa kijiwen na kupata msongo wa mawazo na mwishowe kubwia unga na kuwa na kichwa kama ball fitting mfano jamaa yetu yule aliyetoboagaaaa pua
 
Msilaumu maisha kama amefilisika "kweli" basi lawama apewe yeye mwenyewe Mr. Nice. Watu tunakuwa wa ajabu sana kila kitu lazima tutafute pa kuangushia lawama. Mara "Maisha" mara "shetani" mara "wachawi" kila mtu ana anatafuta pa kuangushia lawama.

Maisha yako ni matokeo ya matendo yako, hakuna wa kulaumiwa zaidi yako mwenyewe. Na wale wanafiki wanaojifanya wanaouliza "cha ajabu kipi" kwa Mr. Nice kufilisika mpaka kufikia kuendesha "boda boda" lazima watakuwa na wanamatatizo kichwani au zaidi ya hapo.

Ni pa kujifunza ukipata pesa usiwekeze kwenye dhima "liabilities" wekeza kwenye mali "asset" zitakazokuletea pesa kukidhi mahitaji ya kila siku. Mkipata pesa ni baloon, mark x, gambe, pamba, wakina Lulu kwanini usije kuendesha boda boda baadae.
Ushauri mzuri. Ahsante kwa kunifunza maana ya liabilities kwa kiswahili-dhima.
 
Back
Top Bottom