Mr Nice: Sina UKIMWI ila nililishwa sumu wakati wa kampeni.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Msanii mkongwe wa muziki nchini Tanzania Mr. Nice ameibuka na kusema kuwa hana maradhi ya UKIMWI kama wengi walivyokuwa wanamzushia ila kilichomsumbua mpaka kufikia kulazwa mahututi hospitali ni kulishwa sumu wakati wa Kampeni katika uchaguzi wa mwaka jana.

Mr Nice ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano na Gazeti la Taifa Leo la nchini Kenya lilifanya naye mahojiano wiki hii katika moja swali ambalo aliulizwa ni kuhusu tetesi ambazo zimesambaa nchini humo kuwa ana HIV.

Mr Nice ambaye kwa sasa anafanya muziki wake nchini Kenya, alikanusha uvumi huo huku akieleza nini kilimkuta mwaka jana mpaka akalazwa hospitali kwa miezi kadhaa.

“Kaka wewe mwenyewe ukinicheki nilivyo fresh nina ngoma kweli?,” Mr Nice alimuuliza mwandishi huyo huku akichek.

“Siugui Ukimwi lakini ni kweli mwaka jana nililazwa hospitali kwa miezi mitatu kuanza October. Nililishwa sumu kali wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hatukuweza kubaini ni nani alifanya hivyo lakini tulijua ni mambo ya siasa na nikamwachia Mungu.

Kwa sasa Nice afya yake imerejea kama kawaida na anaendelea na kazi zake za muziki nchini Kenya.

Katika hatua nyingine amesema Tanzania kuwa na wasanii wengi kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 kuliko jirani zake Kenya na Uganda kulitokana juhudi za msanii moja moja.

“Kusema kweli wasanii wa Tanzania wamekuwa wakishindana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja anataka kufanya kazi nzuri kuliko mwenzake. Kwahiyo binafsi naona hii hali imesaidia kuwajenga wasanii wa Tanzania pamoja na muziki kiujumla,”.

Source: Bongo 5
 
Zile dawa za Ngoma zinasaidia sana.
Leo Mr.Nice amerudi vizuri kiasi cha kuukana kabisa Umeme. Tunakoelekea huenda akaacha hata kunywa zile dawa, kisa asijihisi yeye ni mgonjwa tena, na hapo majanga yatarudi upya.

Sumu anyweshe mwaka jana, story atupe leo?!
Kwa ile hali aliyokuwa nayo kitandani kipindi kile akiugua, mimi nitakuwa mtu wa Mwisho kuamini kuwa ilikuwa ni Sumu. Yaani ilikuwa ni Kidatu kabisa.

Hongera Mr.Nice
 
Tena inakuja sindano ya UKIMWI unachoma mara moja kwa mwaka, wala mambo ya kukutana kwenye kitengo inahusu?
Nilimpereka marehemu kaka yangu pale Amana Hosp katika krinic ya Aids,duu nikakutana na jamaa tunafanya ofisi moja,jioni bro akaniuliza yule jamaa mliosalimiana nae mbona anajistukia?,kila Mara ananitizama?,mwambie ajiweke wazi asiogope...
 
Nilimpereka marehemu kaka yangu pale Temeke Hosp katika krinic ya Aids,duu nikakutana na jamaa tunafanya ofisi moja,jioni bro akaniuliza yule jamaa mliosalimiana nae mbona anajistukia?,kila Mara ananitizama?,mwambie ajiweke wazi asiogope...
Rafiki yangu ni daktari kwenye kitengo, aliniambia usije ofisini tuonane sehemu nyingine yeyote, ukija pale jioni watu wanaanza kupeana habari kuwa na wewe ni muathirika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…