Mkuu ni heri ukawa na bifu na bondia au mcheza karate au mfanya mazoezi yoyote Yule kwani mtaishia kupigana au kupigwa na case ikienda mbali sana ni polisi na kila mtu anarudi uraiani salama
Usidharau na wala usitake kabisa bifu na wala unga au mateja, hao hawana ugomvi wa kupigana ngumi kusema mtapanga speringi mpigane au wakupe nafasi ya kujipanga siku ingine
Bifu na mateja waga lina njia ya mkato tu, na wengi wanapotea kutokana na hizo dharau kama zako, Teja yeye anajua fika Hana uwezo wa kukupiga ata Kofi, atakimbilia kisu/panga au akutoboe toboe na bisibisi
Kumbuka wakati yeye anafanya hilo ni tofauti na mtu mwenye Akili timamu ambae anafikilia nini kitatokea badae, yeye anafanya hilo akiwa hajui nini kitatokea badae ata kama utakufa kutokana na shambulio lake ye hajali
kutokana na dharau kama hizi zimefanya wengi wamepoteza maisha yao au kupata ulemavu wa kudumu au ata kutumia gharama kubwa sana kwenye matibabu ilhali huyo Teja ata afungwe gerezani ye hana alichopoteza
Ni rahisi sana kwao kumpoteza mtu Kwa hela ndogo sana na wengi wanapotea kutokana na kuwadharau kwamba hawawezi kuwafanya chochote, wakishapewa uhakika wa kupata madawa ya kulevya ata kama ni elf 10 tu hawataki kujua kosa lako wala hawataki kujua we ni Nani
Alichofanya Mr touch ni sahihi sana tena zaidi ya sahihi na atakuwa kaambiwa ukweli na watu wanaowajua mateja vizuri, cheed itambidi arudishe majeshi nyuma kama ni kweli kisa hiki ni cha kweli, si polisi wala mwanajeshi anaeweza kukulinda dhidi ya teja hao jamaa kwenye matukio waga Wana speed of light