Mradi gani naweza kuufanya kwa mtaji wa milion 8.?

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,588
Reaction score
22,752
Mwezi wa 9 napata kiasi cha mil 8 sasa nataka nijaribu biashara ambayo itayofanya nisijutie kuiterekeza hela yangu hiyo.NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO WAPENDWA,NDUGU WANA JF.
 
Hua nasikia wanasema kua ununuzi wa mazao unamaslahi sana
 
biashara ziko nyingi, inategemea wewe unapendelea sana kufanya kitu gani, pia ukijaribu kuangalia na kupitia baadhi ya topics mbalimbali zilizotumwa unaweza chagua ile ambayo unaipenda na ambayo unaweza kuona itakurejeshea faida
 
Fuga kuku wa mayai

Kwanza, hawafi hovyo kama wa nyama

Pili, wana faida mara mbili, kwanza utauza na kula mayai then at last wakikoma kutaga utawauza kama kitoweo

Tatu, hawahitaji mtaji mkubwa, unaweza kuanza na mtaji wa 2M
 
Anza na biashara ya nusu mtaji may be 4m ambayo utaisimamia kitovu kwa kitovu. Kama kwenye usimamizi hautasimamia kwa 100% itakula kwako big time..! Forget about hiring someone at the begining
 
Mwezi wa 9 napata kiasi cha mil 8 sasa nataka nijaribu biashara ambayo itayofanya nisijutie kuiterekeza hela yangu hiyo.NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO WAPENDWA,NDUGU WANA JF.

mkuu maelezo uliyotoa hayatoshelezi kwa wewe kupata ushauri wa kukusaidia sana hapa. labda kama haupo serious ama unatest upepo ili ukizikamata izo ela ujue pa kuanzia. kama upo serious weka taarifa za muhimu mfano unapatikana wapi na hata vitu unavyopendelea ili uweze kuchauriwa vizuri.
hapo kwenye red; kama unataka KUJARIBU utajaribu sana na hutopata matokeo mazuri.
 
Nipo Dar nasema kujaribu kwa sababu kuna kufail
 
Mwezi wa 9 napata kiasi cha mil 8 sasa nataka nijaribu biashara ambayo itayofanya nisijutie kuiterekeza hela yangu hiyo.NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO WAPENDWA,NDUGU WANA JF.

... unapata hizo hela kutoka wapi? Je unakopa au ni mafao?
...kama ni mkopo kumbuka marejesho na riba yake, na kama ni mafao au vinginevyo' JIPANGE SAWASAWA...
funguka...
 
Nipo Dar nasema kujaribu kwa sababu kuna kufail

Unapofanya kitu akili yako iweke unafanya shughuli kwa faida na mawazo ya ku-fail unayaondoa kichwani kwani ukiingia kwa kujaribu na biashara itakujaribu pia, maisha tunayoishi ni uchaguzi wetu wenyewe. Ushauri wangu jaribu kuangalia biashara ambayo itatumia mtaji kidogo ikiwezekana theluthi moja ys mtaji ili upate nafasi ya ku-gain uzoefu taratibu taratibu assuming kwamba hujawahi kufanya biashara then unaongeza mdogo mdogo mtaji mpaka unakomaa kwani misingi ya biashara inajengwa na UJUZI NA UZOEFU, MTAJI, SOKO, FAIDA na MATUMIZI YA NYUMBANI hivyo katika kufanya shughuli zako lazima hayo mambo uyaangalie kwa makini
 
hauko serious, kama uko serious funguka zaidi,
1) je kwa sasa unafanya shughuli gani?
2) unaishi mkoa gani na eneo gani?
3) je ni hela ya mkopo? kwa maana kwamba utatakiwa kuirudiasha?
4) kama ni mkopo marejesho yatategemea hiyo biashara au aina nyingine ya kipato?
5) je mda wako ukoje? yaani mda gani uko free na mda gani hauko free?
6) ......
jibu kwanza
 
Du! mpaka sasa wachache tuu ndio waliotoa jibu lakini wengi waliochangia ni bla bla tuu.
Pole mwanzisha mada.
 
Msaidieni mwenzenu je afungue bar sinza? Je afungue mgahawa posta? Je awe mama/baba lishe?
 
Mwezi wa 9 napata kiasi cha mil 8 sasa nataka nijaribu biashara ambayo itayofanya nisijutie kuiterekeza hela yangu hiyo.NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO WAPENDWA,NDUGU WANA JF.

Ziweke fixed deposit mpaka June next year then uingie vijijini ununue hasa mpunga kwani ni rahisi kuhifadhi.Faida ni mata mbili ila usitegemee sana kutuma watu.
 
Fuga kuku wa mayai

Kwanza, hawafi hovyo kama wa nyama

Pili, wana faida mara mbili, kwanza utauza na kula mayai then at last wakikoma kutaga utawauza kama kitoweo

Tatu, hawahitaji mtaji mkubwa, unaweza kuanza na mtaji wa 2M

Amicus unaweza kudadavuka kwa kushusha ka breakdown kdg? Natanguliza shukrani mkuu!
 
Nenda mto ruvu.
Pale pesa ni ya kuzoa kupitia kilimo cha mbogamboga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…