Mradi gani naweza kuufanya kwa mtaji wa milion 8.?

Mradi gani naweza kuufanya kwa mtaji wa milion 8.?

Mwezi wa 9 napata kiasi cha mil 8 sasa nataka nijaribu biashara ambayo itayofanya nisijutie kuiterekeza hela yangu hiyo.NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO WAPENDWA,NDUGU WANA JF.

Yaani shilingi milioni 8 tu unaisubiri miezi miwili yote mpaka September!!!
 
kwani we unasubiri shilingi ngapi? Acha dharau we mbwa unaezitamani hela zangu.Ni ujinga kuwa na chuki na mtu ambae hata hunjui na wala hujawahi kumuona.TO HELL KAMA VIPI Marcopolo
 
Last edited by a moderator:
Mwezi wa 9 napata kiasi cha mil 8 sasa nataka nijaribu biashara ambayo itayofanya nisijutie kuiterekeza hela yangu hiyo.NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO WAPENDWA,NDUGU WANA JF.

Mi nina business yangu ya Stationery na Video library kwa pamoja (ziko two in one) nauza. Value (thamani) ya biashara ni milioni 7 including bidhaa, mashine, computer, printers, scanner, TV screen, meza/kabati ya aluminium n.k. Maelewano yapo pia. Eneo la biashara ni zuri, Mabibo karibu na shule. Sababu ya kuuza ni kwamba nitakuwa shule hivyo usimamizi siwezi kumudu tena. Picha ya duka imeambatanishwa.... Yaani nakuuzia unaendelea na biashara saa hiyohiyo ukitaka.

Mawasiliano 0758397557, 0718174415.
paperclip.png
Attached Thumbnails
 
Fuga kuku wa mayai

Kwanza, hawafi hovyo kama wa nyama

Pili, wana faida mara mbili, kwanza utauza na kula mayai then at last wakikoma kutaga utawauza kama kitoweo

Tatu, hawahitaji mtaji mkubwa, unaweza kuanza na mtaji wa 2M

Ushauri mzuri, lakini hapo unaposema hawahitaji mtaji mkubwa sijakuelewa!!! kuku wa mayai!!
 
kwani we unasubiri shilingi ngapi? Acha dharau we mbwa unaezitamani hela zangu.Ni ujinga kuwa na chuki na mtu ambae hata hunjui na wala hujawahi kumuona.TO HELL KAMA VIPI Marcopolo

Kwa majibu yako hayo, kitu kidogo umepanic namna hiyo we biashara huwezi utapigana na watu ufungwe bure. biashara yataka moyo maana utakutana na wateja kama marcopolo si utamchoma kisu.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna cha usimamizi wala nini unataka kumuingiza Billie mkenge acha hizo ingekuwa inakulipa usingeacha ungeweka mtu mwaminifu aisimamie hiyo biashara maana kila kitu kinaonekana
attachment.php
 
Last edited by a moderator:
Hakuna cha usimamizi wala nini unataka kumuingiza Billie mkenge acha hizo ingekuwa inakulipa usingeacha ungeweka mtu mwaminifu aisimamie hiyo biashara maana kila kitu kinaonekana
attachment.php

Hapo ndipo akili yako imeishia kufikilia na hivyo ndivyo udhaniavyo
 
Basi mwenye wazo ajitokeze si ndiyo umuhimu wa forum au.

Hahaha Billie leo umekuwa mpole,zamu yako sasa,maana humu ukichana ikifka siku yako watu wanakuchana.
Mie nahisi sio kwamba huna wazo,wazo utakuwa nalo ila unataka kuangalia kama kuna mtu atatoa wazo litakalo relate na wazo lako.
Mie natoa angalizo kwamba usiingizi pesa yote kwenye biashara moja,ni hatari sana.Ingiza angalau 3/4 ya pesa kisha itakayobakia iweke kama Capital Back up.
Wataala wamambo ya ujasiriamali wanashauri kwamba usianzishe biashara ya pili kama ile ya mwanzo bado haijawa stable,hayo ni maoni yao ili kukupa tahadhari,lakini mie nilipoanza maisha nilifanya tatu kwa wakati mmoja.
Maana sio kila biashara lazima niisimamie mie,hii itaondoa presha ya bisahara moja kama haitokuwa inafanya vizuri.
Pili lazima ukubali changamoto,na weka wazo kichwani kwmba 8m ni pesa ndodo sana,hii itaku encourage kufanyakazi kwa bidii.
Maana unakuta mtu anamtaji wa 2m basi akili yake ina tune kwamba nipesa nyingi sana,sasa ikitokea tatizo dogo la kibishara basi anaona bora aache kwa hofu.Lakini amini kwamba wapo watu wanapoteza karibia nusu ya mtaji wote lakini hata kama watatoka kwenye ile biashara basi wamejifunza kitu.
Mie ninajamaa wenzangu ambao walifanya biashara kisha wakazikimbia nakufanya biashara nyingine,ila baada ya muda wakarudi kule kule kwa mwanzo kwa kuona kwamba walipokuwa wamekosea wanaweza kurekebisha,unapofanya biashara lazima uijue kwa undani na ukubali kujifunza,usijione bwana kwa kwakuwa unabiashara ila jione mtwana kama mtafutaji,.
Pia tambua mafanikio yako yapo kwa wale wasio na mtaji na wale ambao wanadharauliwa na jamii kwa kuwa hawana kitu.
Mie biashara zangu mbili,yaani ya Matunda,Juices,snacks na biashara ya viungo nilipata wazo kwa jamaa tu yupo maskani.
Kibaya zaidi ni changamoto za kazi yoyote ndio vijana zinatushinda ila wahindi wanaziweza.
Yaani mtu kama 5m akienda hasara ya 3m basi atazua mara amerogwa au biashara ile mbaya,kuna kipindi unapkumbana na changamoto zile kali na ngum sana basi jua mafanikio hayapo mbali,changamoto za awali za kuijua biashara kwa mjasiriamali wa kawaida ni kama mwaka mmoja na nusu,hapo ndio uwe na maamuzi ya kuiacha au kuendelea.
Vijana wengi tumejaa sifa,yaani ukianzisha tu biashara basi ndio sehem ya madem wako kujua ili wakuone wewe ndio King,hapo ujue hiyo ndio sumu yako,maana unatumia kuliko unachoingiza.
We jiulize kwa watu walivyo wa bishi wa jiji la Dar es salaam ni kweli ulitegema kwamba maji ya mifukoni yangenunuliwa?wakati mabomba ya maji yapo tele hadi kwa mamalishe unapata maji bure.Lakini watu walinunua mitambo ya kisasa ya mamilioni ya pesa na kuuza maji ya viroba na yalikuwa yananywewa sana jijini.
Tambua kwamba unapoanzisha biashara yoyote kwanza heshim mawazo yako,80% ya watu wa karibu yako hawataku support na watakukatisha tamaa juu ya biashara yako,na ukiona wengi wamekusupport basi kuwa makini sana.
Angalizo langu ni kwamba watu sikwamba hawana mitaji ila wengi ni waoga wa kupoteza mitaji,na hao ndio wanaotaka biashara ambazo hazina presha ambazo kwa dunia hii hakuna,maana kila unachokifanya wenzio wapo kwenye game zamani.
Lazima uwe mtu wa Kujiripua,unajua wale wauza matunda pale Buguruni sheli wanaingiza hesabu ya kutisha sana kwa siku wakati mtaji wao hauzidi hata elfy 50,000.
Cha kuangali ni kwamba kwanza ridhika na faida ndogo,usione una 8m basi upate faida kubwa ,la,usiige faida anayopata mwenzio kwa biashara ndogo ukalinganisha na wewe.
Mfano Mie:
Namiliki baadhi ya Boda boda,ambapo kila moja inaleta 50,000 kwa wiki,ambapo gharama ya kununua bodaboda ni wastan wa 2,300,000 full,sasa wakati huo kuna mamalishe mwenye mtaji wa laki moja anapata faida kuliko mie.Lakini huwezikusema kwamba mie sifanyi hii biashara kwa kuiga kwamba mwenzangu ana mtaji mdogo anapata kuliko mie,na ndio mungu akaingiza hekma zake kwenye kupata rizki.

Muongozo:-Wewe toa Mawazo hapa yasiozidi matatu kisha watu wakusaidie kuchambua kila mmoja kwa uzoefu wako.
ALL STAY BLESSED
Kama kuna sehem sipo sawa rukhsa kwa wengine kurekebisha
 
Billie,karibu katika kilimo cha ufuta huku niliko,1.unakodisha ekari 5 @70,000 = 350,000,2.kulima ekari 5 @40,000 mara 2 = 400,000,3.Kumwaga 50,000 4.Kung'olea 200,000 5.Kukata na kupiga 300,000.Makadirio ni gunia 6 kila ekari,gunia moja ni kg 160 na DSM kg ni 3000 - 3600.KAZI KWAKO!
 
Back
Top Bottom