Mradi gani unafanyika kwenye bonde la Mkwajuni?

Mradi gani unafanyika kwenye bonde la Mkwajuni?

Buza Kwa Mpalange

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
268
Reaction score
156
Leo katika kuzurura kwangu nikajikuta naelekea Masaki. Nikiwa ndani ya daladala nikajikuta tunapiga Kinondoni lililo bonde la Mkwajuni nimekuta magari yanapanua ule mto huku mengine yakichota mchanga na kupeleka upande wa pili ya barabara.

Je kuna mradi gani unawekwa pale?
 
Mara nyingine kuelewa kinachofanyika katika ujenzi huwa mpaka ujenzi ukamilike
 
Labda wanapanua mto msimu wa mafuriko upo karibu. Nikipitaga pale bonde la Mkwajuni uwa nawaza hivi aiwezekani kupasua barabara ya kitokea pale Jangwani ikaungana na Morogoro road?.
 
Wanauwekea kingo za zege Mto Ng'ombe... Wameanzia Ubungo Kibo Jirani na Flyover ya Kijazi... kupita Ubungo NHC,Sinza,Kijitonyama kwa Ally Maua,Tandale,Magomeni hadi Unapounganika na Mto Msimbazi
 
Labda wanapanua mto msimu wa mafuriko upo karibu.nikipitaga pale bonde la Mkwajuni uwa nawaza hivi aiwezekani kupasua barabara ya kitokea pale Jangwani ikaungana na Morogoro road?.

Inawezekana, inakuwa barabara ya juu ili isiathiri ule mkondo wa maji wa asili chini...

Ila sasa ndugu zako wa Tanroad huwa hawana mawazo hayo. Ndio waliopitisha michoro ya hayway ya Kimara<>Mailimoja pasipokuwa na ama under/over pass kwenye makutano yenye mafuriko ya magari mathalani MbeziMwisho, Temboni, Stopover

1628595496784.png
 
Back
Top Bottom