Naomba mwongozo kwa anaeweza kunisaidia kuanzisha kiwanda cha uzalishaji mbolea hii adimu kuhusu malighafi ipo ya kutosha! Mnisaidie pa kuanzia ili niweze kuandaa mashine, mtaji na jambo lolote ambalo mnahisi litanisaidia kunzisha mradi huu na pia Alie tayari kuungana nami basi nipo tayari.
Mizigo yenye sumu kama kipindupindu! Kuna meneo kama mabibo kule kuna mabwawa ya hzo v2 pia kwa kiduku korea ndio wanatumia hyo sayansi labda wenze2 waliopo huko wa2eleweshe
Samadi ya binadamu imejaa maradhi kibao; kipindupindu, Typhoid, Dysentery, Minyoo kama Hook worms, (safura) nk. isitoshe harufu yake ni mbaya hivyo utaona kwamba handling yake ni gharama kubwa kuliko handling ya Samadi ya ng'ombe nk.
Shida ni gharama zake, ili ufidie hizo gharama ni lazima uuze kwa bei ya juu kuliko bei ya samadi za wanyama ambazo wakati mwingine hupatikana bure tu.
Pia lazima upate kibaki za bwana afya au TFDA kuhakikisha kwamba usalama wa afya unapatikana kwa wafanyakazi wako na watumiaji pia.
Kifupi ni kwamba; ni mbolea inayotakiwa iwe na maandalizi na matumizi strict comparatively kama madini ya Uranium . Ni biashara kichaa so to say. 🤓