Mradi stendi ya Chunya gharama zaongezeka zaidi ya Bilioni 1 na kusababisha hasara kwa halmashauri

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kuchukua hatua za haraka dhidi ya mkandarasi wa mradi wa kituo cha mabasi wilayani Chunya, kampuni ya MJ Contractors, kutokana na kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo.

Amesema ucheleweshaji huo umesababisha ongezeko la gharama na hasara ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, hali ambayo haikubaliki na inapaswa kushughulikiwa kisheria ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo, Malisa amesisitiza kuwa serikali haitavumilia uzembe au ucheleweshaji wa makusudi katika utekelezaji wa miradi ya umma, hasa ile inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mhandisi wa Wilaya ya Chunya, Charles Kwai, amesema mradi huo ulianza kwa gharama ya shilingi bilioni 2.8, lakini gharama zimeongezeka zaidi ya shilingi bilioni moja kutokana na makosa ya kitaalamu pamoja na usimamizi usioridhisha.

Ameeleza kuwa changamoto hizo zimechangia kuchelewa kwa mradi huo na kuathiri utekelezaji wake kwa wakati uliopangwa.

losefu wa uelewa katika masuaa ya ujenzi kwa viongozi wetu unaishia kushambulia vitu rahisi rahisi kutokana kwa sababu za kijinga .
Ujinga si tusi, ujinga ni kutoelewa.

Mtu asiyelewa kanuni na taratibu za ujenzi, jibu rahisi kwake katika martatizo ya miradi, moja kwa moja anafikiri mkandarasi ndiye ana matatizo.

Serikali sasa hivi haina fedha za miradi , hiyo siyo siri
Wafadhili wengi wameyeyuka.
Fedha kutoka serikalini kulipia miradi inatoka kama maji ya drip.
Sasa unategemea mkandarasi afanye muujiza gani?
Tatizo lingine, serikali yenyewe imeanzisha utaratibu wa TRA Exemptions katika miradi, utaratibu ambao ni mbovu kupindukia.
Vibali havitoki kwa wakati na vikitoka inakuwa TRA imechelewesha mradi.
Sasa viongozi hawalioni hilo, kwa kutoelewa wanalaumu tu mkandarasi.
Kutoelewa huku nako kwa viongozi wetu wa serikali kunakera sana.
 
Back
Top Bottom