Mradi uliokwama kwa miaka 24 wafufuliwa rasmi

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Waziri wa Nishati, January Makamba amefika kwenye Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe na kufika kwenye mradi wa kufua umeme kwa Njia ya Maji wa Rumakali (MW 222) wenye thamani ya Shilingi 1.4 Trilioni uliosanifiwa tangu mwaka 1998.

Mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamesema walishakata tamaa ya kuendelezwa mradi huo, Lakini kwa sasa matumaini hayo yamerudi na wanaamini utatekelezwa sababu wananchi hao toka mwaka 1998 walikua tu wakisikia kwamba kuna mradi wa kufua umeme lakini hakukua na mwendelezo au utekelezaji wowote kuhusu mradi huo.

Waziri Makamba amesema >>'Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutekeleza mradi wa Umeme wa Maji ya Rumakali uliopo Wilayani Makete Mkoa wa Njombe ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa kutosha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya Nishati, kuanzia Agosti 1 2022 Wathamini wanakuja kuzungumza na nyinyi kuhusu maeneo tutakayoyachukua juu ya fidia zenu kwenye eneo hili la Kilometa za Mraba 13.2 zitakazochukuliwa na huo mradi' - Waziri Makamba.

Tunaona jinsi serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilivyo na uchu wa maendeleo
 
29 July 2022
Njombe, Tanzania

WAZIRI JANUARY MAKAMBA AJIBEBESHA ZIGO LA MRADI WA UMEME RUMAKALI NJOMBE, MRADI ULIOKWAMA KWA MIAKA 24

Waziri wa Nishati, January Makamba amefika kwenye Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe na kufika kwenye mradi wa kufua umeme kwa Njia ya Maji wa Rumakali (MW 222) wenye thamani ya Shilingi 1.4 Trilioni uliosanifiwa tangu mwaka 1998.

Source : BM24 News
 
Kweli hapa Rais Samia Suluhu amepata msaidizi mchapakazi
Gridi inatakiwa ishibishwe na inatubidi kila Mkoa itengwe ardhi kama Kilometa kumi mraba ziwekwe Solar Panels na zenyewe ziingizwe kwenye Gridi ya Taifa.

Tanzania tuwe na umeme wa uhakika wenye bei nafuu

Wawekezaji wamwagae mitaji yao ili ajira ziwe bweleleee!!

Mama kajifunga kibwebwe Ugali lazma uive.
 
Uwiiiiiii
Mbonaaaaa
Ulaji mwingine.com
Hii nchi arudi mkoloni tutakuwa salama
Kwaiyo wewe haupendi uhuru unataka utawaliwe kikoloni hamjazoea kuona Rais mchapakazi kama Rais Samia Suluhu amepeleaka umeme mpaka vijijini tena kwa bei nafuu kabisa hata kama mtu hana uwezo anaweza kuafford pia ameleta elimu bure maji mpaka vijijini milado mikubwa kamaliza kwa wakati mnataka nii tena watanzania
 
m
Gridi inatakiwa ishibishwe na inatubidi kila Mkoa itengwe ardhi kama Kilometa kumi mraba ziwekwe Solar Panels na zenyewe ziingizwe kwenye Gridi ya Taifa.
Kila chenye manufaa mama atatimiza hii ni serikali ya utekelezaji
 
May 26, 2021​

TANZANIA YAPATA DOLA MILIONI 140 UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME MARAGARASI, KIGOMA​

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO, leo Mei 26,2021, imeingia makubaliano ya mkopo wa Dola milioni 140 kutoka Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB) kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kufua umeme wa megawati 49.5 kupitia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi uliopo Mkoani Kigoma.

Mradi wa Maragalasi utachochea ukuwaji wa shughuli za maendeleo ya kijamii pamoja na kiuchumi kwa wakazi wa Mikoa ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Mradi huu, utahusisha pia uimarishaji gridi ya Taifa itakayorahisisha biashara ya mauziano ya Nishati ya umeme baina ya Tanzania na Nchi majirani.

Aidha gharama za mradi huo kwa ujumla ni takriban Dola milioni 144.14, ambapo Serikali ya Tanzania itachangia kiwango kinachobakia cha Dola milioni 4.14 kukamilisha fedha za Ujenzi wa Mradi huo muhimu kwa Mikoa ya ukanda wa Kaskazini Mashariki na Tanzania kwa ujumla.
Source : TANZANIA YAPATA DOLA MILIONI 140 UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME MARAGARASI
 
May 26, 2021​

TANZANIA YAPATA DOLA MILIONI 140 UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME MARAGARASI​

Sisi hatupingi ila isijekuwa ni Porojo tu. Bomba la Hoima lenyewe Ajira wana CCM ndio mnaopeana CCM nuksi!
 
January 31, 2021​

Njombe, Tanzania

”SASA NI MEGAWATI 580 ZINGINE KUTOKA RUHUDJI NA RUMAKALI” WAZIRI KALEMANI​

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa Mkoani Njombe Januari 30, 2021 amesema kuwa, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya kufua umeme wa jumla ya megawati 580 kwa njia ya maji ambayo ni, Mradi wa Ruhudji na Mradi wa Rumakali yote kwa pamoja ikiwa Mkoani Njombe.

Alieleza kuwa, Mradi wa Ruhudji utazalisha megawati 358 na Mradi wa Ruamakali utazalisha megawati 222 ambapo maandalizi ya ujenzi wa miradi hiyo miwili mikubwa yameanza utekelezaji wake kwa wakati mmoja ikiwemo maandalizi ya Miundombinu wezeshi kwaajili ya ujenzi rasmi wa miradi hiyo.

“Utekelezaji wa Miradi hii ulianza kwa hatua ya kufanya usanifu wa Miradi tangu Desemba 2020 na unakaribia kukamilika. Sasa tunatarajia kuingia hatua ya pili ya kutangaza zabuni ili kuwapata wakandarasi kuanzia mwezi Machi ili ifikapo mwezi Julai wakandarasi wawe wamepatikana na tuwakabidhi rasmi eneo la ujenzi ili waweze kuendelea na ujenzi‘’ alisema Waziri Kalemani

Waziri Kalemani aliongeza kuwa, Miradi yote miwili inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu na hivyo kuongeza megawati 580 katika Gridi ya Taifa ili kuongeza uwezo ambapo kwa sasa Grid ya Taifa ina uwezo megawati 1602 tu.

“Kwa mahitaji ya sasa, Nchi nzima tuna uwezo wa kutumia mpaka Megawati 1400, lakini kadri tunavyoongeza umeme katika Gridi, ndivyo tunavyo hamasisha na kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi toka nje na ndani ya Nchi, hivyo Serikali imeamua kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia miradi hii miwili ya Ruhudji na Ruamakali” alisema Waziri Kalemani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya ameushukuru uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, Wizara ya Nishati na TANESCO kwa kuanza kutekeleza miradi hiyo muhimu kwa Taifa ambayo utafiti wake ulifanyika miaka mingi iliyopita lakini haikufikia hatua ya utekelezaji.

Mhe. Rubirya aliongeza kuwa mbali na miradi hiyo kuwa na manufaa makubwa kwa taifa lakini ni matarajio ya Wananchi wa Njombe kuwa, Miradi hiyo itafungua fursa za uwekezaji mkuba katika Mkoa wa Njombe na maeneo ya jirani.

Niihakikishie Serikali, Wizara ya Nishati na TANESCO kuwa, Mkoa wa Njombe utaendelea na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ya kutunza mazigira ambayo yatawezeha upatikanaji wa maji kwanza kwajili ya Mradi Mkubwa wa Julius Nyerere lakini pia Miradi hii ya Ruhudji na Ruamakali” Alisema Mhe. Rubirya

Kwa upande wa TANESCO, Naibu Mkurugenzi Uzalishaji Umeme, Mhandisi Pakaya Mtamakaya alisema sambamba na Miradi hiyo ya kufua umeme zitajengwa njia mbili za kusafirisha umeme huo za Msongo wa Kilovolti 400.

“Njia ya kwanza itajengwa kutoka Ruamakali hadi Kituo cha Mwakibete Mbeya na ya pili kutoka eneo la Ruhudji mpaka kilipo kituo cha kupoza umeme Mkoani Iringa ili kuwezesha usafirishaji wa umeme huo kuingia katika Gridi ya Taifa na kutumika katika Mikoa mbalimbali nchini” alisema Mhandisi Pakaya.

Akimalizia ziara yake Mkoani njombe Waziri Kalemani ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe kujiandaa kupokea miradi yote miwili pamoja na kuchangamkia fursa zote za kujipatia kipato kutokana na ujenzi wa miradi hiyo huku akiwasihi wananchi wa Mkoa wa Njombe kulinda vyanzo vya maji, kutunza mazingira pamoja na miundombinu yote ya umeme.
Source : ”SASA NI MEGAWATI 580 ZINGINE KUTOKA RUHUDJI NA RUMAKALI” WAZIRI KALEMANI
 
Jamaa kadandia tireni sasa tunaambiwa ni kwa jitihada zake.
 
Gridi inatakiwa ishibishwe na inatubidi kila Mkoa itengwe ardhi kama Kilometa kumi mraba ziwekwe Solar Panels na zenyewe ziingizwe kwenye Gridi ya Taifa.

Tanzania tuwe na umeme wa uhakika wenye bei nafuu

Wawekezaji wamwagae mitaji yao ili ajira ziwe bweleleee!!

Mama kajifunga kibwebwe Ugali lazma uive.
Mama kaamua vijana tupate ajira ndio maana hatakupitia miladi mingi anayotekeleza lazima watanzania wapate fursa kila chenye manufaa Tanzania mama atakifanya we are so proud of her
 
Mimi nilishasema toka awali kuwa namuunga mkono Bi Samia Suluhu yuko sehemu ngumu sana lakini anapambana kama Boxer na ameshaipiga mibaba mingi Knockout!😁
 
Back
Top Bottom