Mradi wa 'Akon City' wafeli, Serikali yachukua eneo baada ya Akon kutelekeza Ujenzi

Mradi wa 'Akon City' wafeli, Serikali yachukua eneo baada ya Akon kutelekeza Ujenzi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Vyombo vya Habari Nchini Senegal vimeripoti kuwa Serikali ya Nchi hiyo imelichukua eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Mji wa Akon ‘AKON CITY’ na kulirudisha mikononi mwake baada ya Msanii huyo maarufu duniani kufeli kukamilisha ujenzi wa mradi huo wa Mji wa kibunifu kama ilivyotakiwa.

1752136372439.png
Mji huo ulipangwa kujengwa kwa kufuata ubunifu wa Miji iliyoonekana katika filamu ya Black Panther lakini kwakuwa Akon ameshindwa kutimiza ahadi hiyo Serikali imeufuta mradi huo na sasa inapanga kuwekeza dola za kimarekani Bilioni 1.2 katika kujenga hoteli na nyumba za kupanga kwa ajili ya Watalii katika eneo hilo lenye utajiri wa fukwe.

1752141858327.png

Serikali ya Senegal ilimpatia Akon ekari 136 za ardhi mwaka 2020 kwa ajili ya kujenga mradi wa AKON CITY ambao ulikusudia kubadilisha Mji wa Mbodiène kutoka Kijiji cha Wakulima na kuwa Jiji la kisasa lenye huduma mbalimbali kwa gharama ya dola za kimarekani bilioni 6 ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi ilipaswa kukamilika mwaka 2023.

Imeelezwa kuwa, August 2024 Serikali ya Nchi hiyo ilimkumbusha Msanii huyo kwa mara ya kuhusu kuanza ujenzi wa mradi huo ambapo kwa muda mwingi mbuzi na ng’ombe waliishia kuubadilisha na kulifanya eneo hilo kuwa eneo lao la malisho.

Aliaune Damala Bouga Time Puru Nacka Lu Lu Lu Badara Akon Thiam maarufu kwa jina la Akon, alizaliwa miaka 52 iliyopita huko St. Louis Missouri Nchini Marekani ambapo pia katika utoto wake aliishi kwa miaka kadhaa Nchini Senegel wanakotokea Wazazi wake, alitoboa kimuziki mwaka 2004 na kujizolea mamilioni ya Mashabiki baada ya kuachia single yake ya ‘locked up’.

==

The singer and his homeland will turn to a more "realistic" project

Akon‘s plan to build a $6 billion Akon City in Senegal, supported by his own Akoin cryptocurrency, is not working out. Even the best-laid plans, amirite?

The 2018 proposal imagined a virtuous cycle of economic investment in the Republic of Senegal. Graphic representations depicted curving skyscrapers, as both singer and country cultivated comparisons to the Wakanda of Black Panther.

Now the BBC has officially confirmed what anyone following the story has long suspected: It’s not going to happen. Instead, the singer and his home country will focus on a more “realistic” project.

“The Akon City project no longer exists,” according to Serigne Mamadou Mboup, the head of Senegal’s tourism development body, Sapco. “Fortunately, an agreement has been reached between Sapco and the entrepreneur [Akon] Alioune Badara Thiam. What he’s preparing with us is a realistic project, which Sapco will fully support.”

Before it was called off, construction had got as far as an incomplete reception building without roads, water, or power.

Akon broke out with his 2004 hit “Lonely,” and subsequent blockbuster singles including “Smack That” with Eminem, “Don’t Matter,” and “I Wanna Love You” featuring Snoop Dogg made him an international star. But you can count on two hands the number of musicians who’ve turned their millions into billions — and despite his accomplishments, Akon would be an opener for all of them.

The scheme always depended on his Akoin becoming the next big cryptocurrency, which would have required better luck — and better financial instincts. “It wasn’t being managed properly,” Akon conceded in 2022. “I take full responsibility for that.”

Since then, Akon has prepared for a return to music, releasing a few 2025 singles ahead of a new album.

Source: consequence.net
 
Angeungana na sadio wangeweza kuikamilisha hio ndoto
 
Kakaa kitapeli tapeli tu ...angetatufa wachezaji mpira maarufu Senegal waigizaji wenye asili ya huko wangekaa pamoja lazima Kuna kitu kikubwa kingewekwa hapo
 
Serikali wameliona eneo baada ya hiyo project?
 
Wasanii sio wa kuwaamini. USD 6b sio mchezo mchezo. Hata angeungana na Sadio Mane bado parefu mno wasingeweza. Serikali ya Senegal iige serikali ya Tanzania kwamba wasanii ni wa kuimba kwenye shughuli za kiserikali tu ikiwemo mikesha ya mwenge. Kuwaamini kwenye mambo nyeti ni hatari kwa Taifa.
 
Serikali ya Senegal ilitakiwa ijue msanii kazi yake ni kuimba kwenye kampeni za chama tawala na sio kumshirikisha kwenye jambo kubwa kama hilo.
Bora sadio mane kajenga shule na hospital,sasa hutu anataka kujenga kitu kwa mawazo ya black panther sijui wakanda
Mradi mbwembwe nyingi tu
Si angejenga sehemu za makazi tu watu waishi

Ova
 
Bora sadio mane kajenga shule na hospital,sasa hutu anataka kujenga kitu kwa mawazo ya black panther sijui wakanda
Mradi mbwembwe nyingi tu
Si angejenga sehemu za makazi tu watu waishi

Ova
Mzee wa Kino USD bilioni 6 yalikuwa mawazo ya ndotoni. Sadio Mane ni mkweli.
 
Trump mwenyewe hana utajiri wa hiyo Bilioni 6 ndiyo ije kuwa AKON? Akon alikuwa anatafuta Kiki na upigaji tu.
 
Back
Top Bottom