Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Hizi nadharia zote zinazoibuka kuhusu huu mradi zinazimwa na maneno mawili tu; UMEOUNA MKATABA, na zaidi haya maneno mawili yanawafaa zaidi wote wanaotaka haya mazungumzo yaendelezwe.
mkataba urapitishwa kila mtaa,wenyeviti wa vitongoji watausambaza kwa kila kaya..πŸƒπŸƒπŸƒ
 
Naomba nikuulize swali la kijinga, Wewe na marafiki zako wawili mkiingia ubia mkafungua biashara ya duka,

Mahesabu ya faida ya duka utamtuma mkeo pekee akafanye mahesabu au mtayafanya wewe na marafiki zako mlioanzisha duka?
 
Huyu nae kwa kuandika ushuzi hajambo!
 
Mnaopinga mradi wa bagamoyo pigeni kimya machozi yenu yaende na maji kama nasi yalivyoenda KILA kitu Chato
 
Naomba nikuulize swali la kijinga, Wewe na marafiki zako wawili mkiingia ubia mkafungua biashara ya duka,

Mahesabu ya faida ya duka utamtuma mkeo pekee akafanye mahesabu au mtayafanya wewe na marafiki zako mlioanzisha duka?
Hapa mataga hawezi kupa jibu
 
Yericko Nyerere aje atupe taarifa mradi wa Bandari Bagamoyo umefikia wapi sisi tumpe taarifa mradi wa JKNHP umefikia wapi.
Watu hawajifunzi tu kwa aina ya viongozi ambao tunao,

Sio watendaji, ni rahisi tu kuzungumzia jambo ili kuwapa matumaini Watanzania , lakini ndani ya mioyo yao , huwa wanajua wanamaanisha nini,

Sasa huyu naye anayejiita Jasusi,

Yaani mtu mwenye taarifa nyeti , naye ni mtu wa kumwamini kweli ? Mpaka ununue kitabu chake, si unatupa pesa yako bure tu,

Watanzania msipende kuingia kwenye mitego kama hii,

Na kwa serikali yetu , ni bora kusubiri kila kitu kama kipo kwenye mipango yenu , angalau kifikie kwenye hatua nzuri ya uhakika wa kufanyika , ndio mtoe taarifa
 
Eeeh! Yericko Nyerere mmefikia wapi na mradi huu wa hovyo uliolaniwa?

Mlilipa pesa kidooogo za watu wa maeneo hayo ya Zinga, Kiromo, mbegani kwa kitu kinaitwa EPZ, pesa nyingi mkatia mifukoni mwenu mkawatimua wenyeji wakaondoka kwa kunung'unika saana,

Mlikuwa mnaandika kwenye cheq milioni 4 kwa mfano, watu wanasaini, mkitoka hapo na cheq zenu mnaenda kuongezea ziro mbili mbele! Halagu mnacjekelea eti mnawakomoa wapumbavu

Sasa kiko wapi? Muwaombe radhi wana Bagamoyo kwanza kwa mlichowafanyia
 
mkataba urapitishwa kila mtaa,wenyeviti wa vitongoji watausambaza kwa kila kaya..πŸƒπŸƒπŸƒ
Uongozi wa juu uliopo ni wa kilaghai kwa mgongo wa demokrasia na watu watakufa sana bila hata kujulikana maana walikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kipindi kilichopita wamewekwa kwapani hawathubutu kutamka chochote maana wameshirikishwa kwenye agano la kugawana mali za umma bila bughudha lakini wananchi waachwa masikini bila mtetezi yeyote mwenye sauti ya mamlaka.

Kipindi cha uchaguzi mtaona ni namna gani chuki mliyoipandikiza itaoneshwa na wapiga kura masikini ijapokuwa mtabadilisha matokeo.
 
Acha visirani, umeandika uzi huu ukimulimwa na MW 270 toka bwawa la nyerere.
 
Huo mradi ushazinduliwa tayari?
Mradi wa bandari Bagamoyo kwa mwekezaji haupo na hautakuwepo. TPA wanajenga wenyewe kwa kuanzia bahari magati kadhaa ili kuanza kupunguza ushushaji wa shehena za mizigo zinazofika bandari ya Dar es Salaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…