Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha


Ni kosa la nani kuficha mikataba? Na isitoshe nani alikuwa anamuamini dhalimu, zaidi ya wajinga na wachumia tumbo?
 
Mkataba umeuona? Lengo lako ni kuuza kitabu feki cha kile unachokiita ujasusi wakati hata tahasusi ya ujasusi wenyewe huelewi

Weka mktaba hapa kila mwenyewe akili kubwa apambanue ukweli ni upi sio blah blah za mwanasiasa ambaye lengo lake ni kujihakikishia himaya.
 
Hivi wewe ushawahi kufanya biashara? Unategemea uwape washindani wako wa biashara proposals zako hadharani.
Kwahiyo ndio umeanza kujitetea kiivi [emoji1787][emoji1787]kwani bandari ni secret formula kama Coca-Cola au
 
Kwahiyo ndio umeanza kujitetea kiivi [emoji1787][emoji1787]kwani bandari ni secret formula kama Coca-Cola au
Project ni kubwa mno ile unafikiri ni karatasi moja? Kuna makampuni na taasisi nyingi sana zimelipwa pesa nyingi zimefanya kazi kufanya upembuzi wa mradi kwa muda mrefu wamewasilisha proposal alafu waitoe tu kwako wewe alafu washindani waone weakness za mradi waje na alternative version ya proporsal waokoe hela ya kufanya upembuzi wao?
Eti secret formula, kumbe hujui?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Haya tetea nchi yako iki inaibiwa mradi wenyewe sio wa watanzania investor ni Oman na China yani watanzania wataona kama pambo
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Haya tetea nchi yako iki inaibiwa mradi wenyewe sio wa watanzania investor ni Oman na China yani watanzania wataona kama pambo
Unajiwazia wewe huoni faida yoyote kwa watoto wa vijukuu vyako kabisa? Au unazani dubai iliibuka tu kama uyoga? Nchi zilizoendelea wanaofaidi matunda hawapo ila walijitoa kwa vizazi vijavyo wewe unaona hasara kwakuwa unajipimia kwa umri wako.acha wajenge hata miaka 99 poa tu. Jamaa lilikua linaongea kwa sababu lilijua miaka 99 halitakua madarakani likapiga chini mradi shwaini kweli yani.
 
Faidi ipi sasa wewe MpK leo accacia umepata faida gani.. Shule 3 zilizojengwa karibu na mgodi.. Mali hiyo ingekuwa tumejenga wenyewe hata kwa pesa za mkopo ingekuwa na maana kinacho chosha zaidi hata ujuzi hutopati kupitia ujenzi huo.. Je in 10 year tunaweza jenga kama hiyo ya bagamoyo pale Tanga kutumia watu wetu. Je kwanini pesa hizo zosingeendeleza bandari ya Tanga kwanini kuwe na bandari za Dar na Bagamoyo karibu swali lengine bandari ya Dar kazi yake itakuwa ni nini. Tanga ndio ingekuwa inafaa zaidi kwasababu ni karibu na mikoa mingi ya kaskazi na kati.
Mkiwa mnashabiki kitu naomba muwe subjective na objective simultaneously sio kuwa na shauku na hisia tuu.
 
Lowasa wakati wa kampeni kupitia UKAWA alisema akishinda urais, mkataba wa hiyo badandari atauvunja na Yeriko alishangilia kauli hiyo ya Lowasa
Labda alikua bado hajauelewa ujasusi wa kidola na kiuchumi unavyofanyika kivitendo tofaut na nadharia anazozijua
 
Kwenye maslahi ya taifa hakuna anaemfikia jiwe....na hapo naamini kwenye hili unamaono madogo..ni suala la muda tu, hata gesi ya mtwara alisikitika sana si yetu tena
 
Ni kweli kwa hili la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na umuhimu wake kwa Taifa kwa leo.
Ila naona una kauli mbili mbili katika mtazamo wako kuhusu ujenzi wa Bwana lá Umeme.

.Mimi sio nabii, lakini angalau nikisema jambo nakuwa nimeona kijacho mbeleni, Naomba nikukumbushe jambo muhimu ambalo niliandika 13 March 2019 katika makala hii chini.

Katika makala hii nilianza kwakusema, "Vita vya Kiuchumi Tanzania chini ya mradi mtambuka wa maporomoko ya Rufiji, siasa ya Mazingira duniani na muundo na mienendo ya Shirika la Elimu, Sayansi na Udhibiti wa Mazingira duniani (UNESCO), vinanipa sababu ya kuiponeza TISS katika ulimbe huu wa vita vya kiuchumi.

Bonde la Rufiji liko kwenye urithi wa dunia kwamjibu wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (UNESCO), Na hivyo ulinzi wa bonde hili ni kwa sheria za kidunia sio kwa sheria za Tanzania, hapa ndipo ambapo nataka kusifu idara za ujasusi na kumsifu Rais Magufuli kwa kuishinda dunia dhidi ya misimano na sera za mashirika haya ya kidunia ambayo Mwalimu yalimshinda, Mwinyi yalimshinda, Mkapa yakamshinda, Kikwete yakamshinda.

Kwa wiki kadhaa nimekuwa nikipitia nyaraka za kijasusi za mashirika na taasisi mbalimbali ulimwenguni (Realiised docs), nimejiridhisha kuwa vita nikubwa kuliko wengi wanavyofikiri, na ikiwa mradi wa umeme bonde la Rufiji utafanikiwa, basi TISS itaingia kwenye historia ya mashirika bora kabisa ulimwenguni kwa counter intelligence hii. Palipo na uthubutu lazima tupongeze.

Awali mradi huu wa Umeme wa Stiegler's Gorge Ethiopia walikubali kujenga, lakini hakuna maelezo kama waliishia wapi ama walishindwa tenda. Zikawepo taarifa za Waturuki kuwa watajenga, nazo zikaishia hewani. Kisha tukashuhudia Arabb Contractors wa Misri wakisaini mikataba ya ujenzi. Bado ujenzi rasmi haijaanza, lakini hatua tu ya kuthubutu kusaini mkataba ni hatua kubwa inayostahili kupongezwa.

Bunge la Ujerumani liliweka azimo kuitaka serikali ya nchi hiyo kuzuia ujenzi wa mradi huo wa Rufiji na badala yake serikali ya Ujerumani isaidie kujenga vinu vya gesi kwaajili ya nishati ya umeme. Kwakuangazia jambo hili watu wengi wanaweza kujiuliza, itakuwaje nchi ya Ujerumani iingilie masuala ya ndani ya Tanzania? Mifumo ya kijasusi iko hivi, kwamjibu wa Nyaraka za idara ya ujasusi ya nchini Lithium (Anual report 2016) inaonyesha kuwa Ujerumani pekee ina majasusi 11 wa ngazi za juu ndani ya UNESCO, na kwa nadharia hiyo, Ujerumani ikitaka kuzuia miradi yoyote yenye uharibifu wa mazingira inatumia msukumo wa UNESCO.

Kinachoweza kutokea ni kuwa UNESCO inaweza kuiandikia barua ya katazo nchi husika kwamba pale ni sehemu ya Urithi wa Dunia (World Heritage site.) na hairuhuriwi kupajenga. Na wanaonya kuwa ukiwa mbishi na ukaendelea kujenga utakuwa black listed. Na kampuni inayopata tenda ya kujenga nayo inapewa barua na kuonywa kuwa itakuwa black listed na Bank Account zako zitakamatwa. Kwakufanya hivyo wanashinikiza kampuni zijitoe katika mradi husika.

Majasusi hawa wamefanya hivyo kuidhibiti Iran, enzi za Reza Khan kwakutumia mashirika haya ya kidunia , ambayo mengi ni mashirika ya kijasusi. Pia nchi za Panama zimewahi kukumbana na nguvu ya mashirika haya.

Kwa namna yoyote naipongeza Serikali kwa ujasiri huu wa kufunga masikio na kelele za kidunia na kuamua kuanzisha mradi huu uliokwamba tangu miaka ya 60+. Hii ni hatua kubwa sana na ninaamini itaacha legacy kubwa sana kwa rais Magufuli na kwa vyombo vya ujasusi nchini ikiwa utafanikiwa, ingawa hakuna nchi au kikundi kilichowahi kushindana na mashirika haya ya kidunia na kikashinda, zaidi ya hapo labda ziwe ni siasa za kura. Bado naamini tumethubutu pakubwa sana, na katika ndoto tutashinda". Makala iliishia hapo.

Sasa mwaka mmoja na baadaa ya makala hii, Kampuni iliyokuwa ikijenga mradi huo imeandika taarifa hii ambayo inajumuisha ndani yake katazo la UNESCO. Isome hapa kwa lugha ya kitumwa....>>> ElSewedy Electric Co - Council on Ethics

Unaweza kujipa nafasi ya kusoma kwa undani zaidi kitabu cha Ujasusi kujua nama Ujasusi dhidi ya Ujasusi unavyofanya kazi na mifano hai toka katika viunga vya dunia ya ujasusi.

Nunua Kitabu kwa Ofa ya Mwezi Mtukufu na #Corona kwa 25,000 tu popote ulipo. Badala ya bei halisi ya 80,000/=

Nunua kwa Mpesa na Tigopesa 0715865544/ 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo.

Kwa Dar kitabu kitaletwa ulipo bure. Nje ya Dar nauli ni 8,000/=
 
Kwa maelezo yako tu, huo mradi ni wa kijinga, yaani bandari ya Dar, Tanga na Mtwara iwe kwa ajili ya bidhaa za ndani tu (ambayo TRA inakusanya mapato) halafu hio bandari ya Bagamoyo ihusike na bidhaa kwenda nje Zambia, Congo, Malawi na Uganda halafu mapato yanakwenda kusokojulikana ( TRA haihusiki)

Uchumi wa TZ kwa miaka mingi unategemea mapato ya bandari kwa biashara ya kimataifa, ndio maana tulijitoa COMESA Baada ya sharti la free trade tukaogopa kukosa mapato ya biashara kimataifa, na sisi ndio lango kuu kwa upande wa bahari ya hindi, kuwakabidhi hayo mapato wachina na waarabu ni ujuha,hapo Kuna harufu kubwa ya rushwa kwa viongozi ili kuizamisha nchi na watu wachache kunufaika.

Acha wachina wajione wajanja kwa kurubuni viongozi wetu uchwala lakini historia itakuja kujirudia
 
Hii ni bandari ya viwanda ya kuleta mali ghafi kwenye viwanda ndio maana inajengwa sambamba na viwanda zaidi ya mia saba na itatoa ajiri rasmi kwa wazawa zaidi ya laki mbili watanzania tuache kupinga kila kitu.
Mlalamika ajiri ndio hizo ajira zinakuja
 
Leo wachina walijaa mtaani kwetu uku bagamoyo wakipima survey kwenye makazi ya watu...ngoja tujiandae kuhama kuwaachia mji
 
Akili ni kile kinachobakia, ukiondoa nadharia na vitendo vyote vya darasani.
Hili jambo mnalishabikia kwa sababu zenu mnazozijua nyie. Umeme ndiyo msingi mkuu wa maendelea kwa nchi yoyote. Jenga bandari kila kona ya nchi kama huna umeme wa uhakika bandari zako ni bure. Umeme wa uhakika ndiyo chanzo kikuu cha wawekezaji kuwekeza katika nchi yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…