Mradi wa Bomba la Mafuta kulikoni?

Mradi wa Bomba la Mafuta kulikoni?

Kaparare

Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
93
Reaction score
234
Maisha ya Tanzania yamejawa na matukio leo uraiani kesho Serikalini kama sio huku basi itatokea Kanisani au kwenye Chama cha Siasa. Bahati mbaya mambo ya msingi hayatiliwi maanani kabisa. Hebu fikiria suala la Tozo za Miamala hatima yake haijulikani. Kama ulimsikia Spika wa Bunge utajua naamanisha nini.

Kuna Fukuto la Katiba linaendelea sio suala la jipya Lakini ukiangalia kwa makini utaona ni watu wasiozidi Mia tatu ndio wanaimba wimbo kuhusu Katiba Mpya wengine labda hawaujui huo wimbo.

Hao Mia tatu wakinyamaza hao wengine wanaoitikia hutowasikia tena na suala hilo litakuwa limepita.

Tuachane na mengine mengi kama ya akina Mbowe na utata kuhusu Ugaidi wake au Samia na mzigo Mzito mabegani mwake. MAANA NI MENGI SANA Lakin tuyaache hebu tuangalie suala Mradi wa wa BOMBA LA MAFUTA Hoima mpaka Tanga.

Mradi huu ni kama ndoto inayokuja na kupotea. Mara ya mwisho ilisemekana wanalipa fidia kwa Maeneo ambayo Bomba/Mradi utapita lakini wenyeji wanasema hawajamuona hata mmoja mwenye majina wala fedha ya kulipa fidia. Kitu pekee kinachosikika tena kwa uchache ni vikao vikao vikao.

Hasira yangu ni kuwa Serikali inajua attention inayoiweka kwa wananchi wake. Kwann mambo hayanyooki vizuri. Waziri Kalemani kwenye utiaji saini pale dar es salaam alisema mambo yamekwisha na watu waende Site/mahali ambako ujenzi unafanyika lakini mpaka sasa hatuoni chochote. Mwenye taarifa na Mradi huu atuambie mwenye swali pia ni ruksa kuongeza.

Naomba nimalize kwa kusema Serikali iliyoomba Kura na iliyoapishwa tu zina utofauti mkubwa hata kwenye Morali ya Kazi na utendaji kwa jumla.
 
Back
Top Bottom