Mradi wa JHNPP umeondoa mgawo wa Umeme

Mradi wa JHNPP umeondoa mgawo wa Umeme

Kama ambavyo sisi hulalamika pale wanaotuhudumia wanapofanya vibaya, basi ni jambo jema la kiungwana kuwakumbuka na kuwapongeza wanapofanya vizuri.

Katika maisha yangu, sijawahi kushuhudia Tanzania ikiwa na umeme unaowaka mfululizo kama mwaka huu 2024 baada ya JHNPP kuanza uzalishaji. Kwangu ni kama ndoto.

Mungu amweke pema jemadari wetu JPM aliyeamua Ku take risk na hongera kwa wenzake wote waliomsaidia kufanikisha hili kama vile:

1. Rais wa sasa toka akiwa VP kwa JPM na hata baada ya kurithi alihakikisha inakamilika.
2. VP Philip Mpango kuanzia akiwa Waziri wake wa Fedha hadi sasa akiwa VP kwa SSH.
3. Aliyekuwa waziri wa nishati Dr. Medard Kalemani. Aliupiga mwingi.
5. NWM Dotto Biteko kwa kukamilisha kwa umakini wa hali ya juu.
6. Mhe. Mwigulu Nchemba
7. January Makamba
8. Makatibu Wakuu Kiongozi wa awamu zote mbili na makatibu wakuu wote
9 Mameneja wa miradi
10. Tanesco wote
11. TRA wote
12. Watanzania wote na wawekezaji kwa kulipa kodi.

Hakika huu mradi ni mradi wa sura ya kitaifa ambao karibia serikali yote ya JMT imeshiriki kwa namna moja ama nyingine. Ni kielelezo cha mradi ulitekelezwa na serikali za marais wawili bila chenga zozote. Inaonyeaha kabisa kwamba kumbe tukivumilia, tunaweza.

Kumbe tukiangalia mbali tunaweza. Mradi huu utaleta athari nyingi chanya katika uchumi Kwa kuhakikisha umeme wa uhakika. Utaleta investment confidence, ujasiriamali, ajira na kodi kwa Serikali.

Changamoto iliyopo mbele yetu kama Taifa hasa vyombo vya ulinzi na usalama ni ulinzi wa mradi huu.
Vijana wa JJ Mkunda hasa wale chini Major General Mkeremy, tuwe macho katika mradi huu zaidi ya kawaida. Kwa sasa huu mradi ndio vital installation yetu pengine kuliko hata JNIA. Huu ni sambamba na Bandar ya DSM.

Vijana wa Balozi Siwa tuwe macho zaidi ya kawaida. Vijana wa Kamishina wetu wa PCCB, tuwe makini.
Serikali pia iwawezeshe vyombo hivi kwa rasilimali Fedha na watu ili iweze kuhakikisha usalama wa vital installation zote kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo.
Anayestahili credit ni Magufuli kwa uthubutu wake.

Mradi huu ulipigwa vita na Muhongo, Zitto na wapinzani wengine na makuwadi wengine waliofisadi gesi
 
Kiangazi kinakuja, andaa andiko la utetezi. Nimekaa pale!
Catchment Area ya Bwawa la Nyerere ni kubwa. Ukame wa kusababisha usumbufu kwa Bwawa la Nyerere sio wa kitoto. Huo ukame utakuwa janga la kidunia.
 
Ngoja nyumbu waje kupinga
Kwa hili Bwawa kila mtu aliyekuwa akilipinga amenywea. Kulipotokea mafuriko walianza kujitokeza kidogo kidogo lakini wamenywea tena. Waliambiwa pia mafuriko haya kusababishwa na Bwawa hilo.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
You will be amaized, tembea hii nchi. Kama kuna watu wa kwanza kuharibu miundombinu ni wabongo wenyewe, suala lanutunzaji bongo ni zito
Labda kama huwezi kuelewa maana ya urefu wa kamba na ndio maana unatupa lawama kwa hao waiba vyuma chakavu tu ila WALIOKO WIZARA ZA FEDHA,UCHUKUZI,MAMBO YA NJE,MALI ASILI,MADINI,NISHATI NA PALE JUU KABISA HUONI WAKIFANYACHO AMA KWAKO WAYAFANYAYO KWAKO NI BARAKA TELE.

ILI TUWE WAADILIFU BASI IWE NI KWETU SOTE.
ISIWE NI KWA WALE TUNAOAMBIWA TUHAMIE BURUNDI TU.
 
Kama ambavyo sisi hulalamika pale wanaotuhudumia wanapofanya vibaya, basi ni jambo jema la kiungwana kuwakumbuka na kuwapongeza wanapofanya vizuri.

Katika maisha yangu, sijawahi kushuhudia Tanzania ikiwa na umeme unaowaka mfululizo kama mwaka huu 2024 baada ya JHNPP kuanza uzalishaji. Kwangu ni kama ndoto.

Mungu amweke pema jemadari wetu JPM aliyeamua Ku take risk na hongera kwa wenzake wote waliomsaidia kufanikisha hili kama vile:

1. Rais wa sasa toka akiwa VP kwa JPM na hata baada ya kurithi alihakikisha inakamilika.
2. VP Philip Mpango kuanzia akiwa Waziri wake wa Fedha hadi sasa akiwa VP kwa SSH.
3. Aliyekuwa waziri wa nishati Dr. Medard Kalemani. Aliupiga mwingi.
5. NWM Dotto Biteko kwa kukamilisha kwa umakini wa hali ya juu.
6. Mhe. Mwigulu Nchemba
7. January Makamba
8. Makatibu Wakuu Kiongozi wa awamu zote mbili na makatibu wakuu wote
9 Mameneja wa miradi
10. Tanesco wote
11. TRA wote
12. Watanzania wote na wawekezaji kwa kulipa kodi.

Hakika huu mradi ni mradi wa sura ya kitaifa ambao karibia serikali yote ya JMT imeshiriki kwa namna moja ama nyingine. Ni kielelezo cha mradi ulitekelezwa na serikali za marais wawili bila chenga zozote. Inaonyeaha kabisa kwamba kumbe tukivumilia, tunaweza.

Kumbe tukiangalia mbali tunaweza. Mradi huu utaleta athari nyingi chanya katika uchumi Kwa kuhakikisha umeme wa uhakika. Utaleta investment confidence, ujasiriamali, ajira na kodi kwa Serikali.

Changamoto iliyopo mbele yetu kama Taifa hasa vyombo vya ulinzi na usalama ni ulinzi wa mradi huu.
Vijana wa JJ Mkunda hasa wale chini Major General Mkeremy, tuwe macho katika mradi huu zaidi ya kawaida. Kwa sasa huu mradi ndio vital installation yetu pengine kuliko hata JNIA. Huu ni sambamba na Bandar ya DSM.

Vijana wa Balozi Siwa tuwe macho zaidi ya kawaida. Vijana wa Kamishina wetu wa PCCB, tuwe makini.
Serikali pia iwawezeshe vyombo hivi kwa rasilimali Fedha na watu ili iweze kuhakikisha usalama wa vital installation zote kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo.
Muda huu nilipo hakuna umeme
 
Tatizo la hii miradi haina good maintanance, juzi nimepita wami, nakuta washaanza kuharibu zile CCTV camera zilizofungwa darajani. Yaani hadi unajiuliza, aliyefanya hivi ana akili kweli..?
tatizo linaanzia hapa!sisi watanzania hatuezi kutunza na kulinda vitu vyetu!utakuta wanaofanya hvo ni wananchi kabisa!wanaiba wanaenda kuuza
 
Back
Top Bottom