John W. Mlacha
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 3,504
- 1,342
usijali, mradi huu ulianza kuongelewa zaidi ya miaka kumi iliyopita, sasa ujenzi umeanza na world bank washatoa hela, ukiangalia kivukoni kazi imeshaanza, tusubiri kwani pia kuna wamiliki daladala ambao wanaona mradi huu utaua biashara yao, viongzi wetu wametufanyia mambo mpka hatuamini wanachokisema, teh teh, nami nasema nasubiri kuona mabasi hayao yanaanza kufanya kazi.
Barabara za bongo zina eneo kubwa katikakti, mfano kilwa raod, sam nujoma road pia haya mabasi hayahitaji barabara kubwa sana,
angalia mfano wa kituo cha mabasi yaendayo kasi,
mifano hii si ya DART, source skyscrappercity forum
inategemeana, siku nyingine tujitahidi kuwasifia wanapofanya kitu kizuri, tukilalamika siku zote wanaweza sema hii mijitu ukifanya usipofanya sawa , bora tusifanye, kwa hili wanadeserve pongezi, tusiwe wachoyo, na tusubiri wamalizie kama walivyoahidihamna lolote...wasanii wanaonyesha sanaa tu
kwa mbaaali pale namuona mwana anakokota
Asante kwa wote.. nimejifunza kitu....... JF ni kiboko!
Msekwa anasema JF si kitu, Bwa ha ha ha
nikweli kabisa... wa bongo wengi wanafikiri ni mabasi yatakuwa yanaondoka speed balaaa.. but haya mabasi yakuwa na vituo vyake maalum kabla ya kufika kituo cha mwisho.. na vile vituo vyake ni rahisi sana mtu kuruka ule uzio .. sasa sijui ustaarabu huu bongo tutauweza au watazidisha uzio. vituo vipo kama hii picha ya chini
hii si mojawapo ya sweet dreams tu?!!
wabongo pia hawajazoea kudumbukiza nauli wenyewe, kama watatakiwa kudumbikiza nauli na hamna konda basi wameuwawa, maana hata huku watu walioendelea huwa wanadumbukiza vitu vya ajabu ajabu, kuna coin flani hivi zinatumika kuchezea magemu, ni kama hela basi unakuta mtu anazo hizo, kila siku anapanda basi anadumbukiza tuu, ila siku hizi wameumbuka maana kama unadumbukiza coin kina kashimo chake, kama sio hela haiingii, ni kudhalilika patupu, teh teh, nadhani wataweka madaraja kama vile lile la manzese, daraja hilo litakuongeza mpaka kwenye kituo, ukishuka unapanda daraja kuvuka barabara itakua salama, ila wakiweka uzio itakua fujo tupu, wabongo wataruka tuu, na kwa nauli itabidi wawe wanatumia kadi, unaweka hela ya mwezi mzima, hapa nilipo unaweza kulipa kila siku ukipanda au ukiona shida kial siku kutembea na vichenji basi unanunua kadi ya mwezi mzima, haijalishi utapanda mara ngapi au ruti gani ili mradi umelipa hela ya mwezi we unagonga tuu kadi na mambo ni shwari.
card system itakuwa bomba! .... ila system ya kujitumbikizia pesa wasijaribu.. teh tehe but ifike kipindi tujifunze ustaarabu wa wenzetu nakumbuka Mh. JK alisema huu ujenzi usitishwe kwa sababu ni kiwanja cha kuchezea watoto! tehehehe! mbona bado unaendelea..?!! nafkiri mh. rais alijistukia amekosea.. na kuna siku nilikuwa naangalia ITV on-line kuna kipindi flani cha michezo kina dhaminiwa na PPF , kuna mdau alikuwa analalamika huu ujenzi unawanyima nafasi ya kufanya mazoezi ya mpira.. kwani kile ni kiwanja cha villa squad (nafkiri), kwa maoni yake ujenzi huu unasaidia kudidimiza maendeleo ya soka na akadai kuwa watu wengi watakufa sababu mabasi yatakuwa yanakimbia sana. nafkiri elimu inahitajika,
Serikali inabidi iwe na kipindi maalum TBC na TV nyengine kuonesha jinsi ya kutumia huu usafiri kama kweli ukiwepo. maana bila wananchi kufahamu matumizi yake itakuwa tafrani nadhani.