Mradi wa mabasi yaendayo kasi (BRT) na Dar es Salaam Rapid Transit (DART)

sijaelewa vile wanavyokuwa wanajenga katikati nondo ndeeefu, ivi ndo wananyanyua barabara, wanatengeneza flyover au wanataka kuijengaje jamani hii barabara?
 
sijaelewa vile wanavyokuwa wanajenga katikati nondo ndeeefu, ivi ndo wananyanyua barabara, wanatengeneza flyover au wanataka kuijengaje jamani hii barabara?

Mkuu hizo nondo ni vituo vya hayo mabasi....kumbuka toka Kimara hadi Kivukoni kutakuwa na jumla ya vituo 27 vya hayo mabasi :hat:
 
Wasipoweka ukuta mkubwa kuikinga hiyo njia ya hayo mabasi na daladala zitatanua humo humo.

Halafu wenyewe wanasema sio mabasi yaendayo kasi ni mradi wa mabasi yaendayo haraka kwakuwa yanaenda spidi ya kawaida tu sema yanapita kwenye njia yake bila bugudha. Hii ikianza nauza mkweche wangu.
 
Halafu mbona mbezi ya Tegeta na upande wa Mwenge haupo kwenye mradi huu? Pili nauli itakuwaje tutaweza kupanda sisi wananchi au ndi nauli ya sh 1000 per route?
 
hizo lugha ni kwa ajili ya kukudivert kutoka kwenye hoja ya msingi ambayo ni mategemeo makubwa wananchi waliyo nayo.

Nikiangalia hiyo ramani ya yanapopita naona wazi kuwa haifanyi covarage hata ya 30% ya matatizo ya usafiri na foleni. Laiti ungechukua picha ya Master Plan ya jiji la Dar es Salaam na wakaboresha (sio kwa viwango vya kimataifa) njia za kuunganisa 'neighborings' ingeweza kuondoa foleni kwa zaidi zaidi 70%
 

Nakubaliana na wewe kwa 100%

Dsm barabara chache na ndogo. Kwa mfano huwa nashangaa sana kutoka Nyerere Rd kuja ilala hadi upite Kawawa au mandela hapo kati hamna njia( nasikia wajanja waliifunga wamejenga majengo). Kutoka Ilala kwenda kigogo hivyo hivyo hapo kati kati hamna njia ya kukatiza.

Huu mji inabidi aje kiongozi jeuri afanye maamuzi magumu aseme, ile nyumba vunja , ile vunja weka bara bara wenye nyumba watajuana na serikali.

Kutoka Muhimbili kwenda kinondoni hamna bara bara wote lazima tupite Jangwani au tupite UN tutokee Selander.
 
Tatizo letu kubwa ni kila mtu kutaka kununua na kuendesha gari lake kila mahala...

Faida ya huu mradi si hiyo barabara ya hayo mabasi pekee, bali hata kule ambako hayatapita (omujubi anaziita 'neighborings'). Ukikamilika daladala zitahamia kule kwenye feeder roads ili kuwasafirisha watu kwenda kwenye vituo vikuu vya DART. Hilo tu litasaidia kupunguza msongamano usio lazima especially city center na Kariakoo. Abiria wa DART watakuwa wanatumia electronic tickets ambazo zitadumu as long as you recharge them (kama LUKU).

Huu mradi pia utasaidia kupendezesha mandhari ya bandari salama....
 
hawajamaliza hata kituo kimoja? ni uzembe ama hakuna pesa
 

Basi wadau leo asubuhi katika pita pita zangu mitaa ya jinan uchina, nimeona kituo hiki na kinafanana kabisa na kama kitakavyokua chetu hapo juu, nilifanya uchunguzi kidogo na mambo yalIkikua hivi
hizi ndio BRT lanes zenyewe, wao wamezungushia kafence kidogo na ni BRT only nimeangalia hata mabasi mengine ambayo ni daladala zao hayapiti hapa yanapita pemebeni







hapa ni kituoni, ndio yanaposimama kushusha na kupakia angalia hapo mlangoni ndio unapogongesha kadi yako au unatumbukiza vijisenti vyako, ukiangalia vizuri utaona nauli ni yuan 1 (1 RMB) ambayo itakua kama 200 na kitu ya kibongo, aka dafu na huyo mwanadada ndio kashagongesha hapo anaelekea kusubiri basi lije, na hapo unamuona msimamizi kituoni ka ajili ya maulizo mbalimbali






Mara basi hilo linakuja





LISHAFIKA KITUONI


LIKALA KONA


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…