Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Zakaria Mwansansu amesema:
Hayo Machinjio yana historia kidogo, Mradi wake ulianza Mwaka 2007 hadi 2009, yakaanza kutumika hadi 2013 kutokana na changamoto kadhaa.
Changamoto ya kwanza ilikuwa maji hayapatikani eneo hilo, pili ni Imani kutokana na kukosewa uelekeo wa Kibla kwa wenzetu wa Islamu.
Mwaka 2023 kulifanyika tathimini ya namna ya kurekebisha hizo changamoto na zilihitajika Shilingi Milioni 14 hadi 24 ambayo tayari imeingia katika Bajeti ijayo ya Mwaka 2024/25.
Pia kuna Mradi wa Maji unaotarajia kukamilika Juni 2024, hivyo changamoto ya maji inatarajiwa kumalizwa.
Gharama iliyotumika katika mradi wa awali bado inau tata, hakuna hesabu kamili, wapo wanaosema ilikuwa Shilingi Milioni 25 na wengine wanasema ni Shilingi Milioni 60.
Mkandarasi aliyekuwa anatekeleza mradi huo alikuwa ametokea Morogoro, alifariki na hivyo vitu vingi vilikwama hapo.
Wakati huo mimi na hata Mkurugenzi wa Uyui wote hatukuwepo hivyo kuna taarifa ambazo hatuna uhakika nazo.
Kuhusu usalama wa nyama inayochinjwa kwa sasa, eneo ambalo mifugo inachinjwa kwa sasa ni mbali kabisa na eneo hilo ambalo mradi wake hautumiki na kuna Wataalam wa Afya wanatekeleza majukumu yao kwa maana ya kufanya ukaguzi.
Pia soma Haya machinjio ya Nyama Wilayani Uyui (Tabora) ni hatari kwa Afya