Mradi wa maji wa miji 28, Mangaka Maji sasa asilimia 100

Mradi wa maji wa miji 28, Mangaka Maji sasa asilimia 100

Wizara ya Maji

Govt Institution
Joined
Oct 2, 2024
Posts
34
Reaction score
20
Mji wa Mangaka na maeneo jirani sasa kunufaika na mradi wa maji wa mji 28 uliofanikishwa na Serikali ambapo hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi ni hakika asilimia 100 kutoka asilimia 20.

Ni hatua mahsusi ya Serikali katika kuongeza uzalishaji na kusambaza maji katika mji wa Mangaka na maeneo ya vijijini vya wilaya ya Nanyumbu yanayopitiwa na bomba kuu, ikiwemo kijijini Masuguru, hivyo kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa maji na hatari ya kuchota maji katika mto wenye Mamba.

Mradi una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni tano (5,000,000) kwa siku na kuhudumia wakazi wapatao 81,000 walioko Nanyumbu mjini na vijiji vinavyopitiwa na bomba kuu. Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji inakuwa asilimia 100 katika mji wa Mangaka.

Thamani ya mradi wa miji 28 Mangaka ni takriban Dola za Marekani USD 16,380,000.59 na Serikali tayari imelipa Dola za Marekani USD 13,497,058.48.

 
Back
Top Bottom