PreGE2025 Mradi wa maji Ziwa Victoria kuelekea Singida - Dodoma, kukamilika Juni 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Serikali inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi mikoa ya Singida na Dodoma, ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2025.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ameeleza hayo leo Aprili 14, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mkalama (CCM), Francis Mtinga, aliyehoji kuhusu mpango wa serikali kuhakikisha vijiji vya Mkalama vilivyoko ndani ya umbali wa kilomita 20 kutoka bomba kuu la mradi huo vinapata huduma ya maji.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akijibu, Mhandisi Kundo amesema mradi huo mkubwa utakapotekelezwa utahudumia miji ya Singida na Dodoma pamoja na vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka bomba kuu, ikiwemo vijiji vya Wilaya ya Mkalama.

Kwa vijiji vilivyo nje ya kilomita 12, amesema serikali inakusudia kuvifikia kwa huduma ya maji kupitia awamu ya pili ya mradi huo baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

Kwa sasa, amesema jumla ya vijiji 29 kati ya 70 vya Wilaya ya Mkalama vinapata huduma ya maji safi na salama kupitia mtandao wa bomba, huku vijiji 41 vikitegemea vyanzo vya maji vya point source na pampu za mkono.

Aidha, serikali inaendelea kutekeleza miradi sita ya maji katika vijiji vya Mbigigi, Isene-Matongo, Mdilika, Tumuli, Singa na Mwangeza, ambayo ikikamilika itanufaisha zaidi ya wananchi 15,000 waishio kwenye vijiji hivyo vya Wilaya ya Mkalama.
 
Serikali inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi mikoa ya Singida na Dodoma, ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2025.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ameeleza hayo leo Aprili 14, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mkalama (CCM), Francis Mtinga, aliyehoji kuhusu mpango wa serikali kuhakikisha vijiji vya Mkalama vilivyoko ndani ya umbali wa kilomita 20 kutoka bomba kuu la mradi huo vinapata huduma ya maji.

Akijibu, Mhandisi Kundo amesema mradi huo mkubwa utakapotekelezwa utahudumia miji ya Singida na Dodoma pamoja na vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka bomba kuu, ikiwemo vijiji vya Wilaya ya Mkalama.

Kwa vijiji vilivyo nje ya kilomita 12, amesema serikali inakusudia kuvifikia kwa huduma ya maji kupitia awamu ya pili ya mradi huo baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

Kwa sasa, amesema jumla ya vijiji 29 kati ya 70 vya Wilaya ya Mkalama vinapata huduma ya maji safi na salama kupitia mtandao wa bomba, huku vijiji 41 vikitegemea vyanzo vya maji vya point source na pampu za mkono.

Aidha, serikali inaendelea kutekeleza miradi sita ya maji katika vijiji vya Mbigigi, Isene-Matongo, Mdilika, Tumuli, Singa na Mwangeza, ambayo ikikamilika itanufaisha zaidi ya wananchi 15,000 waishio kwenye vijiji hivyo vya Wilaya ya Mkalama.
Miradi ya maji, usanifu juu ya upembuzi chini ya usanifu, lakini viwanja vya mpira/stadium arusha na dodoma hakuna usanifu na hela zipo anza kujenga..watu wa dodoma wakiwarudisha ccm mwaka huu, basi uwezo wao wa kufikiri hauko km binadamu wengine wa kawaida, uko chini ya kiwango cha binadamu wa kawaida.
 
Serikali inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi mikoa ya Singida na Dodoma, ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2025.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ameeleza hayo leo Aprili 14, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mkalama (CCM), Francis Mtinga, aliyehoji kuhusu mpango wa serikali kuhakikisha vijiji vya Mkalama vilivyoko ndani ya umbali wa kilomita 20 kutoka bomba kuu la mradi huo vinapata huduma ya maji.

Akijibu, Mhandisi Kundo amesema mradi huo mkubwa utakapotekelezwa utahudumia miji ya Singida na Dodoma pamoja na vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka bomba kuu, ikiwemo vijiji vya Wilaya ya Mkalama.

Kwa vijiji vilivyo nje ya kilomita 12, amesema serikali inakusudia kuvifikia kwa huduma ya maji kupitia awamu ya pili ya mradi huo baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

Kwa sasa, amesema jumla ya vijiji 29 kati ya 70 vya Wilaya ya Mkalama vinapata huduma ya maji safi na salama kupitia mtandao wa bomba, huku vijiji 41 vikitegemea vyanzo vya maji vya point source na pampu za mkono.

Aidha, serikali inaendelea kutekeleza miradi sita ya maji katika vijiji vya Mbigigi, Isene-Matongo, Mdilika, Tumuli, Singa na Mwangeza, ambayo ikikamilika itanufaisha zaidi ya wananchi 15,000 waishio kwenye vijiji hivyo vya Wilaya ya Mkalama.

Nashauri wawe makini sana sana kuna ongezeko kubwa sana na cancer kanda ya ziwa mpaka leo wanaficha ficha sababu ni nini? Je ni kemikali nyingi kwenye maji ya ziwa ?
 
wakati tulivyokuwa a Christian Nation, tulifanya mambo mengi na ya maana sana, nakumbuka B.Mkapa alivyopigania kushindana na egypt na kuanza miradi hiyo miradi yote iliasisiwa na Viongozi Christian na wote hatunao tena …
 
Back
Top Bottom