Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Ndugu wamiliki wa magari, pikipiki, na vyombo vyote vya moto, Utawala umewarudia tena, baada ya kuwapa ile tozo ya kuchangia dawa za kufubaza VVU na zingine nyingi kwenye mafuta, bado wanadhani mnavibunda vya kutosha na kuthibitisha hilo, Aprili 30, 2026, serikali kupitia PPPC na Jeshi la Polisi wamesaini mkataba mkubwa ambao utakugusa wewe moja kwa moja. Kabla ya kufurahi au kukasirika, hebu tuangalie kwa makini takwimu na kinacho ongelewa kuhusu mradi huu.
Mradi Kwa Ufupi:
Thamani ya mradi ni Dola za Kimarekani Milioni 116 (TZS Bilioni 300+), utakaotekelezwa kwa miaka 20. Vituo 40 vya ukaguzi vitajengwa katika mikoa yote 26. Hisa zimegawanywa hivi: Jeshi la Polisi kupitia TPFCS linamiliki 20%, na mwekezaji binafsi MVI Tanzania, muungano wa SAMA Exim DMCC ya Dubai na VIGOR ya Tanzania wanaomiliki 80%. Uendeshaji utasimamiwa na kampuni ya Applus Automotive ya Hispania, teknolojia inatoka Ujerumani.
Mradi mkubwa. Wabia wa kimataifa. Mkataba wa miaka 20. Sasa tuulize maswali ya msingi.
Suala la Usalama Barabarani ni kweli au Kisingizio?
Hoja kuu ya serikali ni kwamba vituo hivi vitaokoa maisha kwa kuondoa magari mabovu barabarani. Hii imekaa vizuri kuisikia. Lakini takwimu za Jeshi la Polisi wenyewe zinasema nini?
Kulingana na takwimu za ajali za mwaka 2022 ni asilimia 3.4 tu ya ajali za barabani zimesabaishwa magari yenye matatizo au mabovu ikiwemo matatizo ya taa:
Kama lengo halisi ni usalama barabarani, tungetegemea uwekezaji mkubwa kwenye mifumo ya kuwajibisha madereva kama, kamera za barabara, ukaguzi wa ulevi, utekelezaji madhubuti wa sheria. Badala yake, tunaona uwekezaji wa Dola Milioni 116 kwenye tatizo ambalo linachangia asilimia tatu ya ajali zote.
Hii haitoi jibu. Inazua swali: Lengo la kweli la mradi huu ni nini?
Mfumo wa uwezaji kwa njia ya PPP
Serikali inasema kutumia mtaji wa sekta binafsi ni jambo jema, kwa kiasi fulani ni kweli. Serikali haitatumia fedha za umma kujenga vituo, haiwezi kupata hasara kwakuwa gharana zinabebwa namwekezaji, lakini uzoefu wa kimataifa utakuja nchini kwetu.
Lakini PPP pia ina upande wake wa pili ambao lazima uzingatiwe:
Mwekezaji binafsi anamiliki 80% ya biashara inayotoa huduma ya lazima kwa kila mmiliki wa chombo cha moto nchini, kwa muda wa miaka 20. Hii si biashara ya hiari kama hoteli au duka. Wewe huna maamuzi, lazima ufike, lazima ulipe, kwa miaka 20.
Hii inamaanisha mwekezaji ana uhakika wa soko la mamilioni ya wateja bila ushindani wowote. Katika mazingira kama hayo, swali la tozo linakuwa zito sana na hadi sasa, hakuna tozo zilizotangazwa hadharani.
Maswali Ambayo Bado Hayana Majibu
Lakini kwa mmiliki wa chombo cha moto, wewe ambaye tayari unabeba tozo za uagizaji, bima, mafuta, na ada za barabaran, mradi huu unaongeza mzigo mwingine bila kuelezwa wazi gharama zake, bila mfumo huru wa usimamizi, na ukijificha nyuma ya kauli ya "usalama barabarani" ambayo takwimu zao zenyewe hazioni kama tatizo ni ubovu wa vyombo vya moto.
Mradi si mbaya kwa asili yake. PPP si mbaya kwa asili yake. Lakini mradi mzuri unahitaji mambo matatu ambayo bado hayajaonekana:
Bila haya matatu, ahadi nzuri za PR zinabaki kuwa maneno tu na mwananchi ndiye atakayebeba gharama bila kuelezwa ukweli.

| S/N | Chanzo | Asilimia (%) mwaka 2022 |
|---|---|---|
| 1 | Uzembe wa dereva | 36.3 |
| 2 | Kuendesha kwa kasi kupita kiasi | 22.2 |
| 3 | Uzembe wa mwendesha pikipiki | 15.1 |
| 4 | Kuendesha kwa jeuri | 8.0 |
| 5 | Kupita kupita | 6.8 |
| 6 | Magari yenye kasoro (Defective vehicles) | 3.3 |
| 7 | Uzembe wa Waendesha baiskeli | 2.1 |
| 8 | Uzembe wa Watembea kwa miguu | 1.7 |
| 9 | Pombe | 1.6 |
| 10 | Vizuizi vya barabarani | 1.3 |
| 11 | Barabara mbovu | 0.7 |
| 12 | Moto | 0.2 |
| 13 | Kivuko cha reli | 0.2 |
| 14 | Mifugo na wanyama | 0.2 |
| 15 | Uzembe wa abiria | 0.2 |
| 16 | Taa za gari | 0.1 |
Kama lengo halisi ni usalama barabarani, tungetegemea uwekezaji mkubwa kwenye mifumo ya kuwajibisha madereva kama, kamera za barabara, ukaguzi wa ulevi, utekelezaji madhubuti wa sheria. Badala yake, tunaona uwekezaji wa Dola Milioni 116 kwenye tatizo ambalo linachangia asilimia tatu ya ajali zote.
Hii haitoi jibu. Inazua swali: Lengo la kweli la mradi huu ni nini?
Mfumo wa uwezaji kwa njia ya PPP
Serikali inasema kutumia mtaji wa sekta binafsi ni jambo jema, kwa kiasi fulani ni kweli. Serikali haitatumia fedha za umma kujenga vituo, haiwezi kupata hasara kwakuwa gharana zinabebwa namwekezaji, lakini uzoefu wa kimataifa utakuja nchini kwetu.
Lakini PPP pia ina upande wake wa pili ambao lazima uzingatiwe:
Mwekezaji binafsi anamiliki 80% ya biashara inayotoa huduma ya lazima kwa kila mmiliki wa chombo cha moto nchini, kwa muda wa miaka 20. Hii si biashara ya hiari kama hoteli au duka. Wewe huna maamuzi, lazima ufike, lazima ulipe, kwa miaka 20.
Hii inamaanisha mwekezaji ana uhakika wa soko la mamilioni ya wateja bila ushindani wowote. Katika mazingira kama hayo, swali la tozo linakuwa zito sana na hadi sasa, hakuna tozo zilizotangazwa hadharani.
Maswali Ambayo Bado Hayana Majibu
- Tozo Zitakuwa Kiasi gani? Hili ndilo swali la kwanza ambalo kila mmiliki wa chombo cha moto anapaswa kuuliza. Ukaguzi huu ni wa lazima, kwa hivyo tozo ni mzigo wa moja kwa moja kwa wasafirishaji wa umma, wafanyabiashara wadogo, na wananchi wa kawaida. Hadi tozo zitakapotangazwa na kuelezwa wazi, tathmini yoyote ya mradi huu itabaki kuwa nusu ukweli.
- Mgongano wa Kimaslahi, Polisi Ni Mbia na Msimamizi Wakati Mmoja Hapa ndipo tatizo zito linaonekana wazi. Jeshi la Polisi lina hisa 20% kwenye mradi huu. Wakati huo huo, Polisi ndio wanaosimamia sheria za usalama barabarani na utekelezaji wake. Hii ina maana kwamba msimamizi wa sheria ana maslahi ya kibiashara katika mfumo anaousimamia.
- Thamani Halisi ya Fedha Kwa Umma
Dola Milioni 116 ni kiasi kikubwa. Katika miradi yote ya PPP, ni muhimu upembuzi yakinifu, makadirio ya mapato, na mgawanyo wa faida na hasara kutolewa hadharani, ili umma uweze kujiridhisha kwamba mkataba huu unalinda maslahi ya nchi na si maslahi ya kampuni peke yake. Hadi sasa, takwimu hizi hazijatolewa kwa umma. - Usawa wa Huduma Kati ya Dar es Salaam na Mikoani
Vituo 40 kwa mikoa 26 ni changamoto ya kiutendaji. Ni lazima kujiuliza: Je, ubora wa huduma utakuwa sawa Mwanza na Dar es Salaam? Je, mfumo utaweza kushughulikia idadi kubwa ya magari bila kusababisha msongamano mkubwa ambao wenyewe unakuwa tatizo?
Lakini kwa mmiliki wa chombo cha moto, wewe ambaye tayari unabeba tozo za uagizaji, bima, mafuta, na ada za barabaran, mradi huu unaongeza mzigo mwingine bila kuelezwa wazi gharama zake, bila mfumo huru wa usimamizi, na ukijificha nyuma ya kauli ya "usalama barabarani" ambayo takwimu zao zenyewe hazioni kama tatizo ni ubovu wa vyombo vya moto.
Mradi si mbaya kwa asili yake. PPP si mbaya kwa asili yake. Lakini mradi mzuri unahitaji mambo matatu ambayo bado hayajaonekana:
- Uwazi wa tozo kabla ya utekelezaji
- Usimamizi huru usio na mgongano wa kimaslahi
- Taarifa za utendaji zinazotolewa hadharani kila mwaka