House4Sale Mradi wa nyumba Simple, Miliki Nyumba Kwa Milioni 12 tu

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
Drone Online Ads tumekuwa kwa muda mrefu tukiwasaidia watanzania mbinu tofauti na ushauri bure wa namna ya kujenga nyumba bora kwa kutumia gharama nafuu. Hii inatokana na uzofu wetu katika ujenzi, timu ya wataalam wa kutosha wanaoshirikiana sambamba na uwezo wa kupata materials ya ujenzi kutoka viwandani moja kwa moja.

Na sasa tumezindua mradi wa nyumba simple , ambapo utaweza kumiliki nyumba yako ya vyumba viwili vya kulala, sebule, jiko na choo cha ndani ambapo utamgharimu mteja kiasi cha milioni kumi na mbili (tzs 12,000,000) ndani ya siku 60 akikabidhiwa nyumba yake.

Nyumba zetu zinakuwa na Mlango mmoja wa grili,mlango mmoja wa mbao, Madirisha matano ya grili makubwa na grili dogo la dirisha la chooni, pamoja na Tanki la kuhifadhia maji la lita elf mbili (2,000) .

Kwa kila mwezi, tunajenga nyumba mbili tu kwa mradi huu wa nyumba simple ili rasilimali zetu zihamie miradi mikubwa.

Hivyo kama wewe unahitaji huduma hii , piga na 0713039875 kupata maelezo sambamba na kuweka oda yako mapema.



 
Asante sana. Kiwanja kina ukubwa gani? Mradi uko wapi? What are the terms of payment?
Kwa hiyo nyumba pichani ni upana wa mita 8 na urefu wa mita 10. Tunashauri ujenge kwenye kona ya kiwanja chako ili baadaye ujenge nyumba kubwa zaidi. Payment, unalipa full mwanzoni
 
Idea nzuri sana...... Hizo za kwenye picha ndio nyumba zenu?
Kiwanja chenu ama cha mteja?
Ndiyo nyumba zzenyewe. Kiwanja cha mteja. Pia akitupa kazi ya kumtafutia tunamshauri atafute kwa kulipia kwa awamu kama vile vya NSSF pale kiluvya au Visiga ili kuokoa pesa taslimu.
 
Malipo yan lipwaje , kabla ya ujenzi tuna andikishana mkataba?
Tunaandikishiana mkataba mbele ya mwanasheria, malipo unalipa yote mwanzoni kwa kuwa tunanunua material ya ujenzi, kiwandani jumla kuepuka mabadiliko ya bei
 
Najua pesa sio kubwa Sana Ila mmboreshe muonekano wa nyumba. Mf hako kapaa ka 2nd photo aisee hapana.

Mwambieni fundi awe mbunifu zaidi kwenye desgning kwa minor resources zilizopo.
 
Mkuu nikushauri Jambo ! Mna idea nzuri pengine !

Lakini picha hazina sukari ya kutosha, zimekaa kienyeji tu ,,,,hazivutii ! Pengine ungepiga picha ambayo nyumba imekamilika rangi kila kitu kwa nje na ndani mtu akaona!


The way mlivoeka tank hapo karibu na ukuta , mmeweka kienyeji Sana ,,,

Anyway, nothing personal !!
 
Najua pesa sio kubwa Sana Ila mmboreshe muonekano wa nyumba. Mf hako kapaa ka 2nd photo aisee hapana.

Mwambieni fundi awe mbunifu zaidi kwenye desgning kwa minor resources zilizopo.
Tutaboresha boss,karibu
 
Thanks boss, tunakusudia simple kweli, ili tutkikukabidhi ,unapanga finishing iweje
 
Nadhani hapo ndio mwisho mkuu. Inawezekana hiyo ndio final product, HAWAKUPIGII RANGI!
 
Nimeangalia msingi wa hiyo nyumba nikapata walakini na hizi mvua unaweza kustahimili kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…