Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Kiranga,Mazee kama information zako ni accurate, umemaliza mjadala.
Jamaa kama kafuata proces sawa na watumishi wengine wa serikali huwezi kumlaumu directly yeye kama Mwinyi.
Kama unataka kulaumu laumu proces nzima ya kuuza nyumba za serikali, ambayo Mwinyi alikuwa kinda low on the food chain. Yeye alifanya kile ambacho watumishi wote tu walifanya. Kwangu mimi hili kama ni la uhakika linamtolea lawama.
Nyumba za serikali si majengo ila ni viwanja. Vile viwanja ni aghali sana kuzidi hata bei waliyonunulia majengo.
Hivi viwanja kama alivyosema August, kuna siku watu watalia machozi ya damu.
Kila mwenye akili timamu, alipopata kile kiwanja/nyumba basi aliuza. Kama kuna mtu ameamua kuwekeza kwenye zile sehemu kwa kweli namhurumia sana. Siku CCM ikianguka, hao jamaa watafukuzwa kama nzi. Sijui wamepata wapi ubabe wa kuamua kujenga vitu kama vile. Uuzwaji wa zile nyumba kila mtu anafahamu kuwa ulifanyika kinyemela. Huwezi ukauza nyumba za serikali.
Anyway, kama kajenga kihalali au la, tatizo ni kiwanja. Na hiki kiwanja, time will tell. Kuna siku ataombwa aondoe jengo lake kwani nyumba za serikali lazima sijengwe hapo. Eti aliuziwa na Magufuli/Mkapa hilo wala halitakuwa jibu. Ni sawa na kununua mali ya wizi huku ukijua ni ya wizi na baadaye unatoa makaratasi kuwa ulinunua kihalali. Sintashangaa kuwa atakayemfukuza anaweza kuwa huyohuyo Magufuli aliyeshinikizwa na Mkapa kuziuza nyumba.
Nawahurumia sana wanaojenga/kununua nyumba maeneo hayo.