Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar

Kiranga,

Nyumba za serikali si majengo ila ni viwanja. Vile viwanja ni aghali sana kuzidi hata bei waliyonunulia majengo.

Hivi viwanja kama alivyosema August, kuna siku watu watalia machozi ya damu.

Kila mwenye akili timamu, alipopata kile kiwanja/nyumba basi aliuza. Kama kuna mtu ameamua kuwekeza kwenye zile sehemu kwa kweli namhurumia sana. Siku CCM ikianguka, hao jamaa watafukuzwa kama nzi. Sijui wamepata wapi ubabe wa kuamua kujenga vitu kama vile. Uuzwaji wa zile nyumba kila mtu anafahamu kuwa ulifanyika kinyemela. Huwezi ukauza nyumba za serikali.

Anyway, kama kajenga kihalali au la, tatizo ni kiwanja. Na hiki kiwanja, time will tell. Kuna siku ataombwa aondoe jengo lake kwani nyumba za serikali lazima sijengwe hapo. Eti aliuziwa na Magufuli/Mkapa hilo wala halitakuwa jibu. Ni sawa na kununua mali ya wizi huku ukijua ni ya wizi na baadaye unatoa makaratasi kuwa ulinunua kihalali. Sintashangaa kuwa atakayemfukuza anaweza kuwa huyohuyo Magufuli aliyeshinikizwa na Mkapa kuziuza nyumba.

Nawahurumia sana wanaojenga/kununua nyumba maeneo hayo.
 
Mkuu, good question.


Hivi lets say mimi ni mtoto wa kiongozi, naandika business plan yangu kisha naenda benki kuomba mkopo.
Loan officer wa benki anaangalia ile aplication anaona last name NZITO! ananipa mkopo kwa sababu ya nguvu ya jina.

Hapo mnaweza mkanilaumu kweli? Au mkasema nimefanya ufisadi?

kama information zako ni accurate, umemaliza mjadala.


Ukisoma post zote hizo utaona ni kupoteza muda kabisa kumjadili Mwinyi kama mtu mmoja. Watanzania wengi hatuelewi umuhimu wa kujadili "Mfumo" tulionao na badala yake tumebaki kushikilia/ kungangania majina ya watu.

Hatuwezi kufika popote kwa kuendelea kuwajadili hawa Watanzania wanaonufaika kutokana na Watanzania kulala usingizi wa pono. Hawa ni wajanja wachache ambao wa wanafuata mfumo uliopo kujitajirisha bila kuvunja kanuni. Kutokana na mapengo yaliyopo kwenye kanuni zetu, ni watu wachache sana wanaweza kujivalisha kengele na kubadilisha kanuni [kwa faida ya wote] iwapo watakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Mtakumbuka kauli ya Kard Pengo aliposema kwa wale wote wanao onekana mstari wa mbele kupiga vita ufisadi; wajiangalie wenyewe kwenye nafsi zao iwapo watapewa nafasi, wasingeweza kuwa mafisadi!!

Mwanakijiji alituambia hapa JF kuwa "tunapenda mambo mepesi mepesi" yuko sahihi kabisa. Tunapenda kujadili watu na matukio.

Ufike wakati tuangalie MFUMO tulio nao...kutoka chini mpaka ngazi ya Rais. Then, tuone iwapo mambo kama haya yataendelea kutokea...


 

Niliwahi kusoma mahali kwamba one of the problems with Africa is that it's politics revolves around personalities and not policies.

This is basically the gist of your above assertion. How true.

Ndiyo maana hata marehemu Kolimba alisema CCM haina dira wala muelekeo, ni mi ego na personalities tu, mpaka sasa tushakuwa na Azimio la Arusha, Azimio la Zanzibar kuondoa la Arusha, na tamko la Kikwete kuondoa Azimio la Zanzibar, tamko ambalo halina uzito wowote ki policy/ sheria. Kwa hiyo utaona usanii usanii na personalities cults tupu. Na sisi kwa kumjadili Mwiny Jr the person, tna play into that game.Ndiyo maana kila siku Mrema this Zitto that, lakini hatujui hata policies za vyama kwenye uhusiano wa kimataifa, information communication technology, security etc.


Tuachane na Mwinyi the person, kama tuna beef tuangalie uuzaji wa nyumba za serikali kiujumla.
 


Mkuu Kiranga,
Naona humfahamu kwa karibu Mzee Timoth Apiyo hadi ukamwita Marehemu.
Mzee hadi leo bado anapumua ingawa anasumbuliwa na moyo na upande mmoja amepooza. Amekuwa akipelekwa South Africa kutibiwa kwani ugonjwa wa moyo bado haumpi kupumua na High Blood Pressure.

Mwisho niseme wazi kuwa Mzee Apiyo baada ya kuona mambo ambayo Mwinyi alikuwa akifanya (kama ambavyo mwenyewe umesema kuajiri na nchi kuendeshwa na mama Sitti Mwinyi), Mzee Apiyo aliomba mwenyewe kwa hiari yake aachie ngazi mapema. Mambo ya uswahili yalimshinda kabisa yaani nchi kuendeshwa kwenye mkeka. Wazee wengi na mwinyi mwenyewe walimuomba walau amalize na Mwinyi term ya kwanza ya Urais. Baada ya kumaliza muhula wa kwanza na Mwinyi, aliondoka Ikulu na hakurudi tena kwenye term ya pili.

Niliona hilo tu tuliweke sawa maana Mzee Apiyo umemsulubu si kawaida, hadi kumuuwa........
 

Kwa hiyo mkuu kosa lake huyu mbwana ni kuzaliwa Mwinyi?
 

Samahani kwa forum na familia ya Apiyo. I could have sworn nimesoma sehemu kwamba Mzee Apiyo amefariki, naweza kuwa nimemchanganya na aide mwingine mkubwa wa Nyerere, au inaweza kuwa nilichanganya habari za umahututi wake Africa Kusini.

Ni kweli simfahamu kikaribu, na hata hao viongozi ambao nina access ya kuwafahamu kikaribu sitaki kuwafahamu kikaribu, maana naweza kuwasemea mbovu face to face nikawa blacklisted kwenye terrorists list ya Tanzania bure.

I may have meandered a lot, but the one point I wanted to make clear ni kumjibu Bubu Ataka kusema kuhusu ukimya wa Mwinyi back then kuhusu matamshi ya Nyerere kwamba Azimio la Arusha lilizikwa, watu wanao buy public demeanor ya Mwinyi wanaweza kusema easily kwamba Mwinyi hakutaka kujibizana na Nyerere tu, na kama hakujibu haina maana kwamba alikuwa anakubali Nyerere alichosema.

In some people's books, that discipline, deference for his predecessor and assertive practicality inaweza kumpa Mwinyi eminence kubwa kuliko anayokuwa afforded everyday.

Kuhusu kuendesha nchi kwenye mkeka and all, what did you expect from a guy who after all had resigned from public life long ago, yaani jamaa hakuwa hata na ambition ya ku put up a resistance (rejea saga ya mauaji ya wazee Shinyanga kwa imani za uchawi yaliyomfanya Mwinyi ajiuzulu Uwaziri wa mambo ya Ndani in the seventies) yuko local local passive fulani hivi, unampa nchi anataka kuwa na audience na wananchi directly kuhusu mirathi na viwanja kama yeye mahakama vile, utafikiri tumerudi enzi za Harun Rashid.

Ndiyo matatizo ya madrasa mengi bila madarasa mengi.
 
Kiranga,

Haina shida maana niliposoma nikashangaa kuwa hii habari sijaisikia na nina mawasiliano mazuri sana na mtoto wake ambaye ni Dr hapa Poland. Pia inabidi uandike Mzee Timoth Apiyo maana hapa kuna bonge la mtu linaitwa Timoth Apiyo pia (mjukuu).

Anyway, tuendelee na mengine. Labda tu kukumbushia kuwa mpeleka habari kwa Nyerere namba moja alikuwa ni Mkapa (nilisikia). Ilikuwa kila kikao cha mawaziri/bunge basi lazima aende kupeleka habari Butiama. Sijui ukweli ukoje maana sikushuhudia zaidi ya kusikia redio mbao.
 
Hapana. Hakuna mahali nimesema hivyo. Ni kutumia influence ya baba yake kupata whatever he got ambavyo asingekuwa Mwinyi asingevipata.

But isn't that human nature? Hata wewe ukiwa na kitu fulani mwanao ata kitumia au utamuambia asitumie jina lako? Au leo hii mkuu mimi mzee wangu anipatie kazi fulani ni kosa?
 
But isn't that human nature? Hata wewe ukiwa na kitu fulani mwanao ata kitumia au utamuambia asitumie jina lako? Au leo hii mkuu mimi mzee wangu anipatie kazi fulani ni kosa?

Baba kutumia jina lake kumpatia mwanae kazi/ deal ni nepotism.

Tofauti hapa hatujaonyesha hili.
 
But isn't that human nature? Hata wewe ukiwa na kitu fulani mwanao ata kitumia au utamuambia asitumie jina lako? Au leo hii mkuu mimi mzee wangu anipatie kazi fulani ni kosa?
MwanaF,
Hata kama ni human nature it hinges on nepotism especially where your father is the servant of the people. Hapa Marekani walipitisha sheria baada ya rais Kennedy kumchagua mdogo wake, Robert, kuwa Attorney General. Mpaka leo Wamarekani wanakubali kuwa he was the best Attorney General of our time and he was duly qualified. Lakini waliogopa kuwa every President can come and appoint their wives, nephews, brothers, brothers in laws kwenye public positions wakapitisha sheria kuwa no more. Kwa hiyo leo Obama hawezi kumpa kazi mkewe, au mwanaye, katika public service no matter how qualified they are. Na Mwinyi hakuwa na haki ya kumpa mwanae nyumba na National Housing just because he is President. Kama hatuna hizo sheria nyumbani labda wakati umefika tuanze kuangalia uwezekano ama sivyo mtakuta uhondo wa nchi umeshikiliwa na wachache tu wenye majina simply because their parents/relatives are holding big public positions.
 
Hawa jamaa zetu wakishapewa vyeo wanakuwa kama wameonjeshwa kula nyama ya mtu. Watataka kuendelea kuila. Dr. Mwinyi kaona utamu wa kuwa na appartments za kupangisha. Kuna taarifa kwamba alitaka kuchukua na eneo lililo mbele ya nyumba ya Mwalimu Msasani akawekewa ngumu. Nadhani ni katika kunogewa kula nyama ..... kwa kujenga chain ya appartments.
 

Jasusi,

Tanzania tunajenga dynasties - only way out of this quagmire ni kupata kiongozi ambaye ni dictator, that's it! There is no other way out of this .... hata upinzani ukiingia madarakani hali haitabadilika.
 
sioni tatizo kwa hili, ila kama sources of funds are undoubtful and can be justified..hili eneo alikuwa na plan nalo siku nyingi nasikia hata office za ile kampuni yao ya simu iliyokufa HITS alitaka iwe hapo....ni muda nimemsikia akijiingiza katika realestate business maana kuna hata eneo moja pale interconsult ali-bid sijajua kama alipata....tusitumie vibaya uhuru wetu wa kujieleza hapa JF basi kila tutakaloona wenzetu wanafanya basi iwe nongwa na tulalamike....huyu jamaa anajiamini sana, wangapi wanamajengo hapa mjini hukuti hata jina la shemeji yake kuficha ID zao? nampongeza sana Dr. Mwinyi kwa jitihada zake.
hawa vijana wa mzee Ruksa mimi nawasifu sana, ni decent halafu wanatumia pia elimu zao kupata wanachopata hata ikiwa kubebwa lakini kuwe na jitihada, tofauti na vijana wengine wa vigogo wanaotaka tu kutumia majina ya wazee wao kupata posho na kupewa rushwa ili wakawaungaishie baadhi ya watu dili zao...
 
The difference is the same. Ungeniambia kuwa Mwinyi alitengeneza hela zake kutoka kliniki yake ya udaktari ningekusikiliza.
 


Huo udecent wa watoto wa Mzee Ruksa,siwezi kuupinga ,maana wengi hatuko karibu nao kama wewe.
Tukumbuke huyu ni Waziri wa Ulinzi,kama anataka kuwa property developer,ilitakiwa aachie ngazi hii.
I believe huyu Dr Mwinyi,yuko kwenye nafasi hii kutokana na baba yake!I might be wrong.
Ningempa heko kama angekuwa pale Muhimbili ili apate u Consultant asaidie watu.
Tumeona how incompetent kwenye sakata ya mabobu !
 
Mods fanyeni kazi yenu. Huyu mtu hawezi kututukana namna hii!

mode atafanya kazi ngapi jamani??unafikiri aoni hii thread!!@@@
msijiongezee vyeo visivyowahusu JF...ana busara zake ndio maana amekaa kmya
akudo
 

But mkuu kuna factors hauja consider kwenye argument yako hapo juu as corrects as it is.

1. Mwinyi mkubwa haja muappoint mwanae in any public position. Mifano yako hapo juu ni ya a sitting president kumuappoint ndugu yake kwenye public position.

2. Hakuna ushahidi ulio tolewa so far kwamba Mwinyi mdogo kapata hizo nyumba illegally directly through his father.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…