AINA ZA NG’OMBE WA MAZIWA
Kuna aina nyingi za ng’ombe wa maziwa ambao hutofautishwa kwa sifa zifuatazo;
-Umbo, mahali alipotokea.
-Rangi ya ngozi
-Uzalishaji wa maziwa nk.
Zaidi kabisa kuna aina kuu mbili ambazo ni; “Bos taurus” na “Bos indicus”.
Bos taurus inahusisha: Friesian, Ayrshire, Brown Swiss, Guernsey and Jersey na wengine wengi kama vile (Red Dane, Swedish Red and White, Holstein Friesian nk.)
Bos indicus inahusisha: Sahiwal, Red Sindhi, Kenana, Criolo, Tharpakar nk.
1. FRIESIAN/FRESHIANI
-Asilia yao ni holand.
-Hutambuliwa kwa kuwa na rangi nyeupe na nyeusi.
-Uzalishaji bora wa maziwa (7800l/mwaka).
-Walikuwa maalum kwa ajili ya kutengenezea “cheese”.
2. AYRSHIRES
-Wanatambuliwa kwa kuwa ana rangi nyekundu na nyeupe.
-Wanatoa maziwa yenye wastani wa fati 4%.
-Huzalisha maziwa yenye fati nyingi (5400l/mwaka).
3. JERSEYS
-Asili yao ni visiwa vya jersey katikati ya Uingereza na Ufaransa.
-Wanatambuliwa kwa kuwa na rangi mtambuka wa nyeusi na kahawia.
-Maziwa 5700l/mwaka.
-Maalum kwa ajili ya utengenezaji wa “butter”.
KUHUSU UNUNUZI WA HEIFER/MTAMBA.
Siku zote hatushauri mfugaji atafute mtamba mbadala kwa sababu zifuatazo;
-Hawapatikani kwa urahisi na kama wakipatikana ni ghali sana.
-Hatari ya kuingiza magonjwa shambani kwako.
-Ugumu wa kufuatilia historia ya wazazi.
-Hakuna mfugaji anaeweza kuuza mtamba wake bora.
JE WAJUA Kila mwaka ng’ombe wengi wa maziwa wanaondolewa katika shamba kwa sababu mbalimbali ???
Zifuatazo ni sababu kuu;
-Uzalishaji mdogo wa maziwa
-Magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambikiza (TB).
-Matatizo ya uzazi
-Kuuzwa au kuchinjwa tu bila sababu maalum.
HIVYO USHAURI NI KWAMBA, SI KILA MTAMBA UNAOUZWA NI BORA HIVYO ZINGATIA SANA KUOMBA TAARIFA NA KUMBUKUMBU ZA MTAMBA PINDI PALE UTAKAPO ENDA KUNUNUA MTAMBA.
Kuhusu upatikanaji wake kwa huko songea sijafahamu ila Njombe kuna shamba moja kubwa la serikali lipo maeneo ya kitulo pale utapata mtamba mzuri kwa bei nzuri..