Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni chini ya kampuni ya China Merchant Holdings inatarajiwa ukikamilika utaifanya bandari hiyo kuwa kubwa zaid barani Afrika kutokana na kuwa na magati yenye urefu hadi kufikia kilomita 20 na kuhudumia makontena zaidi ya milioni 20 idadi ambayo ni kubwa kuliko ile inayohudumia bandari ya kubwa barani ulaya ya ROTTERDAM.
Kando na huduma za forodha, katika eneo la bandari hiyo kutakuwa na ukanda mahsusi wa kiuchumi ( special economic zone)ambao utachagiza mapinduzi ya viwanda nchini
Ni mradi mwingine mujarabu kabisa chini ya Serikali ya awamu ya tano ambao unaenda kuweka kumbukumbu isiyofutika kwani vizazi na vizazi vitashuhudia faida za kukua kwa biashara kwa eneo hilo, upatikanaji wa ajira na kuingizia Serikali mapato ambayo hutumika katika kugharamia huduma mbalimbali ikiwemo za elimu, afya, maji na miundombinu.