Mradi wa umeme uko asilimia 12 tu na umechelewa kwa miezi 8 Dk Mpango asema hataki kusikia kiswahili wala kisingizio

Mradi wa umeme uko asilimia 12 tu na umechelewa kwa miezi 8 Dk Mpango asema hataki kusikia kiswahili wala kisingizio

Shakari

Senior Member
Joined
Jul 6, 2022
Posts
188
Reaction score
570
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ameinyooshea kidole Wizara ya Nishati kutokana na kushindwa kusimamia mradi wa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi ambao umechelewa kwa takribani miezi 8 sasa. Ujenzi wa Mradi huo uko asilimia 12 tu.

Sitaki kiswahili wala kisingizio ikifika Oktoba 2023 Mradi ukamilike na umeme ufike Katavi.

Ziara ya Makamu wa Rais Dk. Mpango Mkoa wa Katavi imekuwa chungu kwa Waziri wa Nishati, Januari Makamba ambaye Wizara yake ndio imelalamikiwa kwa kuchelewesha mradi huo.

Kwanini Miradi muhimu kama hii inashindwa kusimamiwa kimalifu hadi Kiongozi Mkuu wa Nchi kulalamika kiwango hicho?
 
Kama ana huo ubavu aanze kuwawajibisha hao wazembe ili tujue kweli maneno yake yana mamlaka.
 
Ccm bhana ukisikia wanafokeana unaweza sena kweli wana nia njema. Ukute serikali yenyewe inachelewesha pesa kwa kandarasi
 
Back
Top Bottom