Mradi wa uwekaji wa Anuani za Makazi usimamiwe kwa weledi

Mradi wa uwekaji wa Anuani za Makazi usimamiwe kwa weledi

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Pongezi nyingi sana kwa Serikali ya awamu ya 6 chini ya Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu kwa kuamua kufanya zoezi hili muhimu na nyeti kwa usalama wa nchi yetu lakini pia kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Zoezi hili ni muhimu na nyeti sana, ni zoezi mtambuka kwani linagusa kila wizara, kila sekta, hivyo ni muhimu watendaji watakao endesha na kusimamia zoezi hili wakawa ni watu weledi, waaminifu na wazalendo.

Mara zote miradi muhimu kama hii inaharibiwa na watendaji wanao tekeleza huku chini ambapo wakati huo viongozi hawahusiki hapo ndipo mambo huharibiwa.

Chonde chonde ili mradi huu mkubwa ulete maana iliyo kusudiwa basi viongozi wetu wote wafuatilie kwa makini haswa ktk Jiji la DSM ambalo linachangamoto lukuki.
 
Zoezi hili lilianza enzi za Kikwete
Sasa havi kuna maboresho makubwa na ya kitaalamu yamefanyika, ikiwemo.
1. Maboresho ya ramani, itakuwa ya kidigitali.

2. Mfumo wa kutambua kila mtaa.
n.k.
 
MAKAZI HAYA YALIYOJENGWA KIHOLELA ITAKUWA BADO KUNA CHANGAMOTO YA ZOEZI HILI
 
MAKAZI HAYA YALIYOJENGWA KIHOLELA ITAKUWA BADO KUNA CHANGAMOTO YA ZOEZI HILI
uko sahihi lkn wataalaamu wetu watajua nn cha kufanya.

Jambo la msingi wasiachiwe watu wababaishaji.....wakabidhiwe watu makini.

Rais wetu kadhamiria shida ipo ktk usimamiaji.....hivyo ma RC, DC, DED, Serikali za Mitaaa, wenye viti wa mitaa, vyombo vya ulinzi na usalama, mawaziri wote na makatibu wao, na watendaji wote ktk idara mbalimbali wakiamua kujitoa kwa uwezo wao wote zoezi litakamilika kwa ufasaha na kwa 100%.
 
Pongezi nyingi sana kwa Serikali ya awamu ya 6 chini ya Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu kwa kuamua kufanya zoezi hili muhimu na nyeti kwa usalama wa nchi yetu lakini pia kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla.

KWANZA NI KWANINI UNAANZA NA PONGEZI KWA RAIS?
 
Back
Top Bottom