Sielewi labda. Kwa mfumo wa Tanzania ofisi ya mwendesha mashtaka (DPP) si ina mamlaka ya kukataa kuendesha hii kesi?
Kuna point nilizitoa huko kwingine:
Kikubwa ni kupata ushahidi kwamba kweli walitumwa, mara nyingi anaetoa contract au kuwatuma anarekodiwaili kutiwa hatiani. Ataachiwa pale ambapo kunakuwa hakuna ushahidi mahili kwamba alitoa maagizo. Huyo afande alituma watu wakabake, akikana na kusema si kweli, kuna ushahidi gani kwamba aliwatuma? Haiwezi kuwa suala la their word against her word, lazima kuwe na kitu kinaitwa substantiating evidence kwamba aliwatuma, mfano malipo, au walimrekodi nk. La sivyo huwezi kumfungulia mashitaka, anachomoka.
Nyerere alimuuliza mwandishi wa habari Nairobi, tu akikuambia mimi ni baba yako, kwamba nilitembea na mama yako ndio ukazaliwa, utamuamini kwa kuwa tu amesema hivyo?